[wanabidii] MTALII ACHEPUKA NJIA NA KUNASA KILELE CHA MAWENZI KILIMANJARO

Saturday, March 22, 2014

Mtalii kutoka nchini Ujerumani anayefahamika kama Bi. Jeanne Traska (32) akiwa na muongoza wageni Athuman Juma leo majira ya saa mbili na nusu asubui wamekwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro kwa kamba iliyonasa na kuwafanya wasiweze kushuka chini wala kwenda juu.


Bi. Jeanne Traska na Athuman Juma walianza kupanda mlima kupitia Kampuni ya Nordic Tours tarehe 18.3.2014 kwa kutumia njia yaRongai - Kibo –Marangu safari ambayo ingewachukua siku tano. Hadi sasa taarifaza awali zinaonyesha kuwa Bi. Jeanne alitakiwa kwenda kileleni Kibo lakini katika mazingira yasiyofahamika alibadili uamuzi na kuelekea kilele cha Mawenzi ambacho huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.


Shirika la Hifadhi za Taifa kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours wanaendelea na jitihada za uokoaji kwa kutumia askari ambao wanaelekea eneo la tukio pamoja na helikopta itakayosaidia zoezi la uokoaji kwa kutegemea na hali ya hewa itakavyotulia ambapo hivi sasa kuna mawingu mazito katika eneo la mlima.


Umma utaendelea kufahamishwa maendeleo ya jitihada za uokoaji kadri zitakavyopatikana.


Imetolewana Idara ya Mawasiliano

Hifadhiza Taifa Tanzania

22.03.2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments