[wanabidii] Maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni

Tuesday, March 25, 2014
Mafundi wa Kampuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisuka nondo katika moja ya nguzo zitakazoshika daraja hilo



Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigambonio Bw. Lin Tao kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) akionesha jinsi ambavyo daraja la kigamboni litakavyoonekana baada ya kukamilika. Kulia kwake ni Mratibu wa Mradi kutoka Wizara ya Miundombini Bw. Hussein Mativila. Daraja hilo kutoka Kurasini mpaka Kigamboni takribani kilometa moja litakuwa na njia sita kwa ajili ya magari. Daraja hili linajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka kwa Bw Lin Tao (katikati) kulia kwake (mwenye tai nyekundu) ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za Uzalishaji. Wa kwanza kulia (mwenye suti nyeusi) ni Meneja wa Mradi kutoka NSSF, Bw Karimu Mataka

Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za Uzalishaji, Bw. Maduka Kessy akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa daraja la Kigamboni. Mbele yake ni Menaja wa Mradi kutoka Kampuni ya ujenzi wa daraja hilo (CRCEG-MBEC JV)

Moja ya nguzo inayosukwa katikatika ya maji ya bahari huku kukiwa na bomba la pembeni linalotoa maji nje ya eneo linalosukwa nondo na zege kali.

Mhandisi wa Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Aldelsomond Elthag kutoka Arab Consulting Engineers (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy (mwenye tai nyekundu), kulia kwake ni Mhandisi Omari Athumani kutoka Tume ya Mipango wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.

Mafundi wa Kampuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisuka nondo katika moja ya nguzo zitakazoshika daraja hilo.

Picha zote: Joyce Mkinga,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments