[wanabidii] Bunge la Katiba Lina Mamlaka ya kutoifuata au kubadili Rasimu nzima, Muundo na mamlaka ya Serikali ya Muungano

Wednesday, March 26, 2014
Swali la kujiuliza kwa wajumbe wa bunge maalum: Inawezekana vipi kuwa na serikali ya Shirikisho (Muungano) yenye nguvu chini ya mfumo wa serikali 3?. Katika mfumo wa sasa wa serikali mbili, wajiulize Rwanda na Burundi zikitaka kujiunga zitabaki na serikali zao na Tanganyika iendelee kutokuwepo? Au zitaendelea kubaki serikali mbili ya Zanzibar na Muungano huku ya muungano ikijumuisha Rwanda, Burundi na Tanganyika?. Wajumbe wa bunge la katiba wakiweza kujibu maswali haya basi watapata ni serikali zipi za muungano tuwe nazo na mamlaka yapi ipewe serikali ya muungano kwani muungano wetu ulilenga umajumui (pan Africanism) ambao haupo kwa sasa.

Nisema tu kwamba Bunge la Katiba linayo mamlaka ya kuandika katiba mpya bila kufuata rasimu, kufuta ibara au kuongeza ili mradi tu katiba watakayoiandika iende mbali kuliko rasimu ya katiba, historia inaonyesha hivyo. Na majibu ya maswali hapo juu ni mamlaka inayopewa serikali ya Muungano ya juu kuliko serikali za washirika. Mamlaka ya serikali ya muungano yote ili yatekelezwe yatategemea serikali ya Muungano kupewa mamlaka ya kutoza kodi. Huu ndio wasiwasi aliouonyesha Rais Kikwete na kuamua kuupigia debe mfumo wa sasa wa serikali mbili.

Niseme tu serikali 3 zinawezekana na si gharama kama Rais Kikwete anavyodai ila alichofanya ni kutumia mapungufu ya rasimu ya katiba kutoweka wazi mamlaka ya Serikali ya Muungano juu ya utozaji kodi. Tatizo la tume ya warioba na Rais Kikwete ni kutofanya tafiti sehemu nyingine zenye shirikisho ambazo ndo nchi zilizoendelea kuliko nchi zenye serikali mmoja juu ya mapato. Mfano wa nchi zenye serikali nyingi yani zenye kufuata mfumo wa shirikisho ni Marekani, Japan, Ujerumani, Russia, India, Afrika Kusini na Australia. Nchi hizi si kwamba zina mifumo ya shirikisho kwa sababu pengine ya serikali za washirika kuwa tayari kutoa michango yao kwa serikali kuu au Utajiri. 

Nchi hizi zililenga kujenga dola yenye nguvu inayotokana na nchi huru kama Marekani na kuondoa uwezekano wa utawala wa kidikteta, mgawanyo wa madaraka na kuleta ushindani wa ubunifu na utekelezaji wa sera, kupunguza migogoro na kuimiza demokrasia.

Rais Kikwete anaelekea amefanya utafiti wa Mabunge ya Katiba ingawa kwa manufaa yake kuwa na mamlaka ya kufuta ibara, kuzirekebisha au hata kuandika katika mpya na kuipeleka kwa wananchi. Wanaopinga mamlaka haya Bunge Maalum la katiba ni uoga wa kuibuka katiba yenye kiwango cha chini kuliko rasimu ya katiba. Niliangalia kipindi cha This Week Perspective, TVT, Dr Lwaitama alisema Bunge la Maalum linaweza kuifanyia chochote rasimu kwa nilivyomuelewa ila katiba watakayo ileta kwa wananchi iwe na kiwango kuliko rasimu ya katiba. Wasiwasi wa wengi ni kwamba wanayafahamu yaliyomo kwenye rasimu lakini hawaelewi mwisho wa katiba itayoletwa na Bunge la Katiba itakuwa na maudhui yapi.

Ngoja nitoe historia ya katiba ya kwanza kuandikwa duniani na inayopendwa na raia wake zaidi miaka 200 sasa. Marekani ni jamhuri ya shirikisho la jamhuri za nchi huru 50 yani majimbo 50 ( 50 states) lakini ilianza na nchi 13 mwaka 1776 kwa muungano wa mkataba (confederation) na katiba yao inayojulikana kama Articles of Confederation au Articles of Confederation and Perpetual Union iliyopitishwa na bunge la mpito la nchi 13 zilizoanzisha Marekani mwaka 1777. Katiba hiyo badae ilipelekwa kwenye nchi hizo 13 kupitishwa na kufikia mwaka 1781 ilikuwa imepitishwa na nchi zote 13.

Mwaka 1789 katiba hiyo ya shirikisho la mkataba (confederation) la Marekani ilifutwa na katiba ya sasa ya Marekani mwaka 1789 baada ya kupitishwa mwaka 1788. Mchakato wa katiba ya Marekani 1787 haukulenga kuandika katiba yao ya sasa bali Bunge maalum la katiba (Philadelphia Convention ) lilikuwa na jukumu la kuifanyia marekebisho katiba ya Shirikisho la Mkataba kama nilivyoieleza mwanzo, lakini baadhi ya wajumbe na waasisi wa Marekani wakawa na shauku ya kujenga dola ya shirikisho lenye nguvu. Ili kuwa na dola ya shirikisho lenye nguvu, njia ilikuwa moja tu: kuondokana na dola ya shirikisho la mkataba. 

Kwa kuondokana na Shirikisho la Mkataba la Marekani, walikuwa wanaenda kinyume na kilichowapeleka kwenye Bunge la Katiba cha kuboresha shirikisho hilo kwa kuifanyia marekebisho katiba yake " Articles of Confederation". Hivyo wajumbe kwa kuangalia tofauti za mifumo ya shirikisho na matatizo waliyokuwa nayo waliamua kuandika katiba mpya inayofuta dola ya shirikisho la mkataba na kuanzisha dola ya shirikisho la kudumu (federation ) mwaka 1788 ambayo ndo Marekani ya leo na katiba yao.

Kwasababu walikuwa wanaandika katiba mpya kwa kwenda kinyume na waliowatuma kuwawakilisha Bunge Maalum, katiba yao ililenga kushawishi kuungwa mkono na nchi hizo 13 pia kuzishawishi nchi nyingine zijiunge na shirikisho hilo. 

Waliweka katika katiba sura ya haki za binadamu "bill of rights", serikali za washirika zilipewa mamlaka ya kujiamulia mambo yanayogusa raia wake jinsi wanavyoona inafaa, waliweka mfumo wa ugawanaji mapato na wabunge, na jinsi ya kulinda nchi ndogo zenye idadi ndogo sana ya watu kama Vermont. Walianzisha mfumo mpya wa mahakama na kuigawa katika kanda "circuit courts". Katiba ililenga kuweka mgawanyo wa madaraka (separation of power ) wa mihimili mitatu. Serikali ya Shirikisho ili kuweza kutekeleza majukumu yake ilipewa mamlaka ya kutoza kodi kwa viwango vya kodi kupitishwa na bunge.

Waasisi wao waliandika katiba kipindi ambacho ndo zama za kudadisi "enlightment" zilikuwa zimepamba moto, mfano mgowanyo wa madaraka, dola ya jamhuri yenye utawala wa kuchaguliwa na yenye kupata mamlaka toka kwa wananchi walichukua kama ilivyo toka kwenye falsafa ya Charles Montesquieu miaka 20 tu baada ya kuchapishwa. Kutenganisha dini na dola (serikali) falsafa ya Voltaire, Haki za binadamu (haki, umiliki mali, nk ) falsafa za John Locke. Yote haya yalilenga kuvutia nchi nyingine zijiunge na kweli yalifanikisha kwani kutoka nchi 13 mpaka nchi 50 yani majimbo 50 ya Marekani ni kielelezo na ndio maana wanaipenda katiba yao.

Nimetoa maelezo kuonyesha kwamba kama bunge maalum wataenda hatua mbele zaidi ya rasimu basi mamlka ya kufanya hivyo wanayo hata kama wataandika katiba mpya. Kama watazingatia haki za binadamu, mgawanyo wa madaraka, maadili ya viongozi na kuwawajibisha viongozi, na kero nyingine ambazo zinaweza kuondolewa kwa katiba imara basi wafanye hivyo. Lakini kama wataenda chini ya kiwango 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments