[wanabidii] ZITTO MSALITI, MAMA SLAA MZALENDO!

Friday, February 07, 2014
NIMEKUWA kimya kwa muda sasa, nikitafakari mgogoro wa uongozi ndani ya Chadema. Lakini baada ya kimya kirefu, sasa nimeona name nijitokoze ili kueleza kile ninachokifahamu.

Kwanza, nikiri kuwa nimeshutushwa na taarifa kwamba Zitto Zuberi Kabwe, yuko mbioni kusambaza CD zinazokikashifu Chadema mikoani. Nasema siungi mkono mradi huu kwa asilimia 1000.

Siungi mkono kwa sababu, mradi huu wa Zitto umelenga kudhoofisha Chadema, na kwamba kukidhoofika Chadema ni kutaka kukinufaisha CCM. Hili ni jambo chafu na ambalo halikubariki na wapenda demokrasia nchini.

Pili, Ni kiri kwamba ni kweli baadhi ya tuhuma zilizoekezwa kwa Zitto Zuberi Kabwe, siyo za kupika. Zipo za kweli.

Hata hivyo, zipo tuhuma nyingi za kupika zilizosukwa kwa ustadi mkubwa na Jack Zoka yule mkurugenzi wa usalama wa taifa ili kufanikisha mradi wake wa kuisambaratisha Chadema.

Mpango huo ameusuka kwa njia mbili kubwa. Moja kupitia kwa Zitto mwenyewe wakimwambia Chadema ni watu wa baya na wanataka kukumaliza hata maisha yako.

Pili, kupitia kwa Dk. Slaa na Mbowe kwa kuwajaza uongo kwamba Zitto anataka kuivuruga Chadema.

Ujumbe kwa Dk. Slaa unapitia kwa mkewe Mama Slaa ambaye ana uhusiano nzuri na Askofu Gwajima ambaye ni swahiba mkubwa wa Zoka. 

Tabia hii ya Mke wa Dk. Slaa kutumika kuleta mifarakano Chadema haikuanza jana wala juzi.

Kwa mfano, alitumika kuanzisha na kukuza mgogoro wa Karatu kwa kumtuhumu mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Masay kuwa ni mfuasi wa Zitto na hivyo anamhujumu mumewe asigombee urais. Mgogoro uliishia kundwa kwa tume ambazo hazikusaidia hadi mwenyekiti Mbowe mwenyewe kwenda Karatu kutafuta suluhu.

Hadi sasa, mgogoro huo bado unafukuta chini kwa chini kwa sababu ya kuchochewa na Mama Slaa.

Huyu mama amekuwa hachunguzi maneno ya kusema. Amekuwa mropokaji na mara nyingi amekiingiza chama kwenye mgogoro; ikiwamo ule wa Kawe dhidi ya Mh. Mdee.

Dk. Slaa ameelezwa hili mara nyingi sana, lakini kwa kuwa anamsikiliza mkewe na kwa kuwa huyu mama hajui alifanyalo, basi anaendeshwa kama Kondoo.

Kama yupo anayebisha kuhusu hili, aje hapa aseme ili nishushe nondo.

Hivi tukiweka hapa matendo ya viongozi wengine wa Chadema akiwamo Mama Slaa, Mbowe na Slaa mwenyewe, nani atakayepona?
Naye Mbowe ujumbe hufikishwa kwake kupitia kwa baadhi ya mawaziri akiwamo William Lukuvi kwa kisingizio cha wanaitakia mema Chadema. 

Kimsingi mtu makini hawezi kufurahia chama kila siku kinafukuza watu kwa kisingizio cha "usaliti." 

Walianza kuwafukuza madiwani wa Arusha, baadaye wakahamia Kahama sasa wamekuwa Mwigamba, Zitto na Dk. Kitila Mkumbo.

Kiongozi makini hupenda kubaki na jeshi lake; hata kama wengine ni wagonjwa. Kwa mtaji huu, Slaa hawezi kuwa rais na sababu ni kumuendekeza huyu mkewe.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments