[wanabidii] TAARIFA RASMI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Friday, February 07, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

UTANGULIZI
1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.

2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na 
(iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.

3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-

(i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii) Taasisi za Kidini (20)
(iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv) Taasisi za Elimu (20);
(v) Watu wenye Ulemavu (20);
(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix) Vyama vya Wakulima (20); na
(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).

4. Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
5. Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

6. Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.

7. Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:



Na.Kundi/Taasisi Taasisi zilizoleta mapendekezoIdadi ya Watu Waliopendekezwa Idadi ya Wajumbe WanaotakiwaIdadi ya Walioteuliwa
TanzaniaBara ZanzibarTanzaniaBara ZanzibarTanzaniaBara Zanzibar
1.Taasisi zisizokuwa za Kiserikali 246981,203444 20137
2. Taasisi za Kidini5517344 8520137
3.Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu2114 12969422814
4.Taasisi za Elimu9 984462013 7
5.Makundi ya Walemavu 246974320 137
6. Vyama vya Wafanyakazi20189 1319136
7.Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji81 4341073
8.Vyama vinavyowakilisha Wavuvi7 34512107 3
9.Vyama vya Wakulima 2281154420 137
10. Makundi yenye Malengo Yanayofanana14221613 11420146
Mapendekezo Binafsi-- 118-
Jumla672 1782,880874201 13467
Jumla Kuu 8503,754



8. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
9. Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203,wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a) Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijanawatu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b) Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c) Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.
Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:


TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Magdalena Rwebangira2. Kingunge Ngombale Mwiru
3. Asha D. Mtwangi4. Maria Sarungi Tsehai
5. Paul Kimiti6. Valerie N. Msoka
7. Fortunate Moses Kabeja 8. Sixtus Raphael Mapunda
9. Elizabeth Maro Minde10. Happiness Samson Sengi
11. Evod Herman Mmanda12. Godfrey Simbeye
13. Mary Paul Daffa
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Idrissa Kitwana Mustafa2. Siti Abbas Ali
3. Abdalla Abass Omar4. Salama Aboud Talib
5. Juma Bakari Alawi 6. Salma Hamoud Said
7. Adila Hilali Vuai
TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Tamrina Manzi 2. Olive Damian Luwena
3. Shamim Khan4. Mchg. Ernest Kadiva
5. Sheikh Hamid Masoud Jongo6. Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela
7. Magdalena Songora8. Hamisi Ally Togwa
9. Askofu Amos J. Muhagachi 10. Easter Msambazi
11. Mussa Yusuf Kundecha12. Respa Adam Miguma
13. Prof. Costa Ricky Mahalu
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Sheikh Thabit Nouman Jongo2. Suzana Peter Kunambi
3. Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu4. Fatma Mohammed Hassan
5. Louis Majaliwa6. Yasmin Yusufali E. H alloo
7. Thuwein Issa Thuwein
VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)
TANZANIA BARA (28)
1. Hashim Rungwe Spunda2. Thomas Magnus Mgoli
3. Rashid Hashim Mtuta4. Shamsa Mwangunga
5. Yusuf S. Manyanga6. Christopher Mtikila
7. Bertha Ng’angompata 8. Suzan Marwa
9. Dominick Abraham Lyamchai10. Mbwana Salum Kibanda
11. Peter Kuga Mziray12. Isaac Manjoba Cheyo
13. Dr. Emmanuel John Makaidi14. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
15. Modesta Kizito Ponera 16. Prof. Abdallah Safari
17. Salumu Seleman Ally 18. James Kabalo Mapalala
19. Mary Oswald Mpangala20. Mwaka Lameck Mgimwa
21. Nancy S. Mrikaria22. Nakazael Lukio Tenga
23. Fahmi Nasoro Dovutwa24. Costantine Benjamini Akitanda
25. Mary Moses Daudi 26. Magdalena Likwina
27. John Dustan Lifa Chipaka28. Rashid Mohamed Ligania Rai
TANZANIA ZANZIBAR (14)
1. Ally Omar Juma 2. Vuai Ali Vuai
3. Mwanaidi Othman Twahir 4. Jamila Abeid Saleh
5. Mwanamrisho Juma Ahmed6. Juma Hamis Faki
7. Tatu Mabrouk Haji8. Fat –Hiya Zahran Salum
9. Hussein Juma10. Zeudi Mvano Abdullahi
11. Juma Ally Khatibu 12. Haji Ambar Khamis
13. Khadija Abdallah Ahmed14. Rashid Yussuf Mchenga




TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA
1. Dr. Suzan Kolimba2. Prof. Esther Daniel Mwaikambo
3. Dr. Natujwa Mvungi4. Prof. Romuald Haule
5. Dr. Domitila A.R. Bashemera6. Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa
7. Prof. Bernadeta Kilian 8. Teddy Ladislaus Patrick
9. Dr. Francis Michael 10. Prof. Remmy J. Assey
11. Dr. Tulia Ackson12. Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
13. Hamza Mustafa Njozi
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Makame Omar Makame2. Fatma Hamid Saleh
3. Dr. Aley Soud Nassor4. Layla Ali Salum
5. Dkt. Mwinyi Talib Haji6. Zeyana Mohamed Haji
7. Ali Ahmed Uki
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Zuhura Musa Lusonge2. Frederick Msigala
3. Amon Anastaz Mpanju 4. Bure Zahran
5. Edith Aron Dosha6. Vincent Venance Mzena
7. Shida Salum Mohamed8. Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.
9. Elias Msiba Masamaki10. Faustina Jonathan Urassa
11. Doroth Stephano Malelela 12. John Josephat Ndumbaro
13. Ernest Njama Kimaya
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Haidar Hashim Madeweyya2. Alli Omar Makame
3. Adil Mohammed Ali4. Mwandawa Khamis Mohammed
5. Salim Abdalla Salim6. Salma Haji Saadat
7. Mwantatu Mbarak Khamis
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
TANZANIA BARA (13)
1. Honorata Chitanda2. Dr. Angelika Semike
3. Ezekiah Tom Oluoch4. Adelgunda Michael Mgaya
5. Dotto M. Biteko6. Mary Gaspar Makondo
7. Halfani Shabani Muhogo 8. Yusufu Omari Singo
9. Joyce Mwasha10. Amina Mweta
11. Mbaraka Hussein Igangula12. Aina Shadrack Massawe
13. Lucas Charles Malunde
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1. Khamis Mwinyi Mohamed2. Jina Hassan Silima
3. Makame Launi Makame4. Asmahany Juma Ali
5. Mwatoum Khamis Othman 6. Rihi Haji Ali
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1. William Tate Olenasha2. Makeresia Pawa
3. Mabagda Gesura Mwataghu 4. Doreen Maro
5. Magret Nyaga6. Hamis Mnondwa
7. Ester Milimba Juma
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1. Said Abdalla Bakari2. Mashavu Yahya
3. Zubeir Sufiani Mkanga
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1. Hawa A. Mchafu2. Rebecca Masato
3. Thomas Juma Minyaro 4. Timtoza Bagambise
5. Tedy Malulu6. Rebecca Bugingo
7. Omary S. Husseni
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1. Waziri Rajab2. Issa Ameir Suleiman
3. Mohamed Abdallah Ahmed



VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Agatha Harun Senyagwa2. Veronica Sophu
3. Shaban Suleman Muyombo4. Catherine Gabriel Sisuti
5. Hamisi Hassani Dambaya6. Suzy Samson Laizer
7. Dr. Maselle Zingura Maziku 8. Abdallah Mashausi
9. Hadijah Milawo Kondo10. Rehema Madusa
11. Reuben R. Matango12. Happy Suma
13. Zainab Bakari Dihenga
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Saleh Moh’d Saleh2. Biubwa Yahya Othman
3. Khamis Mohammed Salum 4. Khadija Nassor Abdi
5. Fatma Haji Khamis6. Asha Makungu Othman
7. Asya Filfil Thani
WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (14)
1. Dr. Christina Mnzava2. Paulo Christian Makonda
3. Jesca Msambatavangu4. Julius Mtatiro
5. Katherin Saruni6. Abdallah Majura Bulembo
7. Hemedi Abdallah Panzi 8. Dr. Zainab Amir Gama
9. Hassan Mohamed Wakasuvi10. Paulynus Raymond Mtendah
11. Almasi Athuman Maige12. Pamela Simon Massay
13. Kajubi Diocres Mukajangwa14. Kadari Singo
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1. Yussuf Omar Chunda2. Fatma Mussa Juma
3. Prof. Abdul Sheriff4. Amina Abdulkadir Ali
5. Shaka Hamdu Shaka 6. Rehema Said Shamte


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Februari, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments