[wanabidii] TAARIFA KUHUSU MWENYEKITI WA CHADEMA SOMBETINI KUHAMIA CCM

Friday, February 07, 2014
TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANANA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHADEMA KATA YA SOMBETINI BW. ABDI MADAVA KUHAMIACHAMA CHA MAPINDUZI

Ndugu waandishi wa habari, wananchi hususani wakaziwa Kata ya Sombetini, wapenzi na wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mkoani Arusha na taifa kwa ujumla. Baadhi yenu mnafahamu kuwa siku ya jana Alhamis ya Februari 6, 2014 aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Maendeleo Kata ya Sombetini, Bwana Abdi Madava alijitangaza rasmi kuhamia Chama Cha Mapinduzi katika mkutano wa Kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho Sombetini, uliofanyika uwanja wa Mila mtaa wa Simanjiro, Kata ya Sombetini.

Kama mojawapo ya mikakati ya baadhi ya watu wanaoendelea kushirikiana na wapinzani waCHADEMA kukihujumu chama, Bw Madava ametoa shutuma kadhaa dhidi ya chama na viongozi,jambo ambalo sisi kama vijana watiifu na waadilifu kwa chama tumeona sio vyema kuliachalikabaki hivyo bila kueleza ukweli halisi wandugu yetu huyu na ushirika wake kama kiongozi wachama kabla ya kuamua kuondoka.

Ndugu wananchi,baadhi ya tuhuma ambazo ni maneno ya sio ya kweli aliyowaambia wana Sombetini jana na kwamba ndio sababu zilizo mfanya kujiondoa CHADEMA nipa moja na;
Kwamba yeye Madava alijeruhiwa na bomu lililolipuliwa kwenye Mkutanowa CHADEMA nakuua watu waeneo la Soweto – Kaloleni,Jijini Arusha mwaka jana mwezi wa sita na kwamba chama hakikumsaidia lolote.

Kwamba Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema hakuna chochote alichokifanya zaidi ya kuandamana
Kwamba mgombea udiwani aliyepitishwa nachama (Bw Ally Bananga) ni mzigo na kwamba hataweza kuwatumikia wananchi.
Hivyo basi Barazala Vijana CHADEMA (BAVICHA) Kata ya Sombetini linapenda kusema yafuatayo;
Uamuzi wa Bw.Abdi Madava kuhamia Chama Cha Mapinduzi(CCM) umetokana na kisasi na hasira za kushindwa kupata kura kumuwezesha kuwa mgombea wa chama kuwania Kata ya Sombetini. Katika uchaguzi wa kuteua mgombea wa chama, Madava alipata kura mbili tu moja ikiwa ni yake kati ya kura 64,ambapo mshindi alikuwa ni Ndugu Ally Bananga aliyepata ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama Kata ya Sombetini na hadi sasa Bananga ameonesha kukubaliwa na zaidi ya 90% ya wapiga kura wa Sombetini jambo linaloashiria ushindi wa kishindokwa CHADEMA siku ya uchaguzi Jumapili Februari 9, 2014.

Mbali na kuwa na hasira za kukosa uteuzi, Madava amekuwa na malumbano na mgombea mteule (Bananga) na zaidi viongozi wenzake wa Kata pamoja na uongozi wa chama Wilaya kwa sababu ya kushindwa kwenye rufaa yake ndani ya chama.Tangia hapo amekuwa ni mtu wa visasi na ni wa hujuma kuhakikisha Bananga anashindwa kuwa Diwani. Chama ngazi ya Kata kiligundua hili mapema kikamuita kumuhoji lakini hakutokea kikaoni na hivyo ikaamuliwa kumuweka kando kwenye mchakato wote wa usimamizi na uratibu wa uchaguzi kwa upande wa CHADEMA.

Kuhusu kujeruhiwa na bomu na kutopata msaada wa chama. Ninyi nyote ni mashahidi na mna ambavyo chama, wapenzi wachama na wadau mbalimbali walivyojitolea kwa hali na mali kusaidia majeruhi wote na hatawaliofikwana mauti bila kujali cheo cha mjeruhiwa. Hakukuwa na ubaguzi wala upendeleo katikakusaidia wahanga wote. Hatujui yeye alihitaji msaada wa namna gani. Tunafahamu amewahikuibua hoja kwamba apewe nafasi ya kuwa Diwani kwasababu tu alijeruhiwa na bomu lakini kwasababu ndani ya Chadema nafasi za uongozi hazitolewi tu kama zawadi,hakupata nafasi hiyo.

Kuhusu tuhuma kwamba Mbunge wa Arusha Mjini hakuna alichofanya zaidi ya kuandamana. BAVICHA tunatambua tuhuma hizi nimuendelezo wa progaganda za wapinzani wa CHADEMA, sio kwa Mbunge wetu pekee balini taifa zima. CHADEMA kimeendelea kuimarika siku hadi siku mbali na shutuma lukuki kwasababu wananchi wanaonana kuthibitisha nia thabiti ya chama kuleta mageuzi makubwaya kimfumo katika taifa hili. Mbunge wetu ameweza kutimiza mengi kati ya aliyoahidi wananchi mbali na kuvuliwa ubunge kwa hila na kushindwa kuwatumikia wananchi kwatakribani miaka miwili.

Kuhusu tuhuma kwamba mgombea aliyepitishwani mzigo na kwamba hataweza kuwatumikia wananchi. Tunapenda kusema kwambakwanza tunamshukuru Bw Madava ametambua na kukiri kuwa ushindi kwa Ally BanangaKata ya Sombetini ni wa wazi na hivyo ameanza kutoa dosari za kiutendaji kabla hatahajaapishwa na kupewa ofisi. Tuwa hakikishie kuwa Ndugu Ally Bananga ni chaguo sahihikwa chama na atawatumikia wananchi kwa uwezo wake wote na chama hakitamuacha pekeyake.Tuhuma hizi zinashabihiana na hasira na chuki

Kwahiyo BAVICHA Kata ya Sombetini hatumtambui tena Bw Abdi Madava kama mwanachama nakiongozi wa CHADEMA kwa mujibu wa Katiba ya chama Ibara ya 5.1.6 na 5.4.5zinazoeleza kukosa sifa ya kuwa mwanachama wa CHADEMA kwa kuwa mwanachama wa chama kingine.

Imetolewana
KatibuMwenezi (BAVICHA) Kata yaSombetini
Mozec Joseph
7 Februari 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments