Kikwete aishtua Kambi ya Lowassa
Na Njenga wa njenga
KAULI ya rais Kikwete aliyoitoa kwenye mkutano wa baraza la vyama vya siasa lililokutana juzi kujadili maadandilizi ya bunge la katiba,kwamba watu wasiishie kubishana kwamba ni serikali tatu au mbili badala yake watazame na sifa zamgombea imeishtua kabi ya Lowassa.
Kikwete alionenkana kuwashangaa wale wanaishia kubishana kwamba katiba mpya itambue serikali mbili au tatu badala ya kutazama masuala ya msingi ambayo yatakuja kuleta shida wakati wa utekelezaji wake.
"suala hapa siyo kubishana kwamba ni serikali tatu au mbili …yapo mambo mengi ya msingo ambayo kama msipoyaangalia yatakuja kuleta shida wakati wakuitekeleza katiba hiyo……………..kwa mfano rasmi inasema muda wa kugombea ubunge ni vipindi vitatu na mgombea urais sharti awe na sifa ya kugombea ubunge kwanza hivyo unaweza kukuta umewekeza kwenye urais ikifika kipindi unakwenda kuchukua fomu ya urais unaambiwa kuwa huna sifa unaanza kuilaumu katiba mpya……
……..
Hiyo ndio kauli inayotafsiriwa sawa na kurusha jiwer kwenye kichanga cha suala ambapo kila suala hutoka kwa kasi kwani ilionekana kumlenga Sahawia Lowassa ambaye kwa mjibu wa Rasimu ya katiba mpya kama itapita ilivyo hatakuwa na sifa ya kugombea urais kwasababu hatakuwa na sifa yakugombea ubunge baada ya kuvuka vipindi vitatu ya kugombea ubunge.
Hiyo ndio kauli ambayo imeawaamsha wafuasi wakeambao ni wajumbe wabunge la katiba kuapa kuipigania hadi ibadilishwe…
0 Comments