[wanabidii] ATHARI ZA KAULI YA RAIS JK KATIKA MCHAKATO WA KATIBA

Friday, February 07, 2014
Na Julius S. Mtatiro

Jana Rais Kikwete alikutana na wakuu wa vyama vya siasa na kutoa ushauri wake kwao juu ya maridhiano ya kitaifa katika bunge la katiba.(Mimi nilikuwa na majukumu mengine hivyo sikuhudhuria).

Ukiachilia wabunge 357 wa bunge la jamhuri na wawakilishi 81 wa Baraza la wawakilishi watakaoshiriki katika Bunge la katiba, patakuwa na wajumbe wengine 201 wanaotarajiwa kuteuliwa na rais na majina yao yanaweza kutangazwa leo.

Rais amesisitiza kuwa hata hawa 201 atakaowatangaza leo wana mielekeo ya kisiasa yanayotokana na vyama wanavyovipenda na kuviunga mkono kwa uwazi au kwa siri kwa hiyo hawatofautishi na wale wabunge na wawakilishi ambao ni wanasiasa - Katika hili nakubaliana na Rais.

Kwa sababu hiyo Rais ameshauri kuwa misimamo ya kivyama ya sera za vyama inaruhusiwa katika bunge la katiba kwa sababu waliomo ni wanasiasa lakini viongozi wanapaswa kujengeana hoja na kukubaliana bila kukwamisha mchakato huu - katika hili natofatiana mawazo na rais.

Kwa mtazamo wangu, rais amefungua PANDORA BOX, rais anajua wazi kabisa kuwa misimamo ya kivyama ikiruhusiwa na kuchekelewa kidogo tu TUTAVUNA MABUA.

Rais wetu anajua kuwa tukienda kushindanisha misimamo ya vyama tunatoa nafasi kwa chama chenye msimamo fulani na kina uwakilishi mkubwa kupitisha katiba kwa maslahi ya chama hicho.

Nilitegea Rais atajitenga na misimamo ya kivyama walau katika hatua hii ya katiba, nilitegemea Rais ataeleza kinagaubaga kuwa kila anayekwenda katika bunge la katiba lazima kwanza afikirie Taifa linataka nini, wananchi wanataka nini, wananchi wamesema nini - MASLAHI YA TAIFA NI NINI!
Badala yake mkuu wetu wa kaya ameishia kusisitiza kuwa twende na misimamo ya vyama vyetu lakini tuwe makini isitukwamishe.

Yani unawakabidhi watu wenye mitizamo tofauti Bunduki na risasi halafu unawaambia wawe waangalifu kuzitumia, unategemea nini!!! Wakishindana kwa hoja watahamia kwenye Bunduki na walio wengi watawaua wachache na kupitisha hoja wanazozitaka.

Mahali popote duniani mabunge ya katiba hupaswa kujikita hasa katika kufikiri taifa linataka nini siyo chama changu kinataka nini.
Ufunguzi wa PANDORA BOX hili utapelekea chama chenye wajumbe wengi wa bunge la katiba kipitishe misimamo yake na wajumbe wachache wenye hoja muhimu na wanaotaka KATIBA YA WANANCHI wakwamishwe.

"Ni Tafsiri yangu tu".

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments