[wanabidii] Tuwasikilize CCM tupate bora KATIBA? au Tuwapuuze tukose yote?

Thursday, January 09, 2014
semi wa Kiswahili kwamba, 'Mwaga mboga nimwage ugali' unaweza ukapata maana kwa kutafsiri sehemu ya hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Desemba 30, mwaka jana baada ya kukabidhiwa
Rasimu ya Pili ya Katiba. Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete alitoa hadhari yenye sura ya vitisho kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba kuwa iwapo watashindwa kukubaliana katika vikao vya Bunge hilo na kusababisha Watanzania kuyakataa mapendekezo ya Katiba Mpya, lawama zitakuwa kwao na Katiba iliyopo itaendelea kutumika.

Kwa kauli hiyo, Rais Kikwete ni kama 'alinawa mikono' akisema yeye kazi yake imekwisha, wakati chama anachokiongoza ndicho kinadaiwa kuwa na mipango inayokwenda kinyume na mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu hiyo. Msimamo wa haraka wa vyama vya upinzani katika
kupitisha mapendekezo hayo ni pamoja na kusimamia hoja zote zenye masilahi kwa Watanzania na kupinga hoja za kadhaa za chama tawala, CCM.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanatafsiri kauli ya Rais Kikwete kama njia ya kujiweka kando na athari zozote zitakazojitokeza iwapo katiba hiyo haitapishwa. Wachambuzi hao wa masuala ya Katiba wanajenga hofu kwa kauli hiyo ya Rais Kikwete na kuonyesha
mitazamo mbadala itakayosaidia kumaliza mapema uwezekano wa kutokea mvutano usiokuwa wa lazima.

Mwenyekiti wa Baraza la Katiba la Zanzibar, Profesa Abdul Sharrif anasema Katiba ni lazima ipitishwe kwa hoja zenye masilahi ya Watanzania na siyo vitisho kwa vyama vya upinzani. Anasema kauli hiyo ya Rais siyo sahihi kwani Bunge hilo pia litakuwa na wajumbe kutoka CCM ambao wana misimamo yao inayodaiwa kuwa na masilahi kwao na ndiyo wengi.

Profesa Sharrif anasema wanasiasa wote wazingatie ushauri wa Rais Kikwete, wasiangalie masilahi yao binafsi na kupunguza mivutano ili kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana.

Mvutano ni lazima Hata hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally anasema wajumbe wa Bunge hilo siyo lazima kukubaliana na kwamba hatua ya mvutano haitakwepeka. Bashiru anaongeza kuwa rasimu hiyo ni mapendekezo tu ambayo yametolewa na Tume, hivyo wajumbe hao ndiyo watakuwa na nguvu ya kujadili na kufanya marekebisho.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments