[wanabidii] TATIZO NI BEI YA UMEME

Wednesday, January 08, 2014
Watanzania wenzangu nashangaa tulipoambiwa tutalipa kodi ya line zetu za simu tulipiga kelele kwa pamoja mpaka ile kodi imeondolewa.
Vipi mbona umeme umepanda sana bei tumekaa kimya? tumeridhika au ni woga wetu? kweli kama umenunua umeme mwezi huu utaelewa ninachosema, kwani maisha yatakuwa magumu mara dufu bidhaa zote zitapanda bei na majiko yetu ya umeme yatabakia mapambo majumbani mwetu. Hata gesi nayo imepanda bei, mafuta ya taa nayo usiseme halafu serikali inapiga kelele tutunze mazingira wanataka tupikie mchanga?  kama siyo kukata miti ili tupate kuni na mkaa wa kupikia? Hatuwezi kuandamana kwa hili tukafanikiwa kama lile la line za simu?

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments