[wanabidii] Taarifa ya CCM kuhusu kikao chake cha Januari 13, 2014 mjini Zanzibar

Tuesday, January 14, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekuwa na kikao cha siku moja leo tarehe 13/01/2014 mjini Zanzibar chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Kikwete.

  Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wazanzibari na watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepongezwa 
kwa maandalizi mazuri na ya kufana ya sherehe hizo.
 
Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.

  Aidha Kamati Kuu imemteua Ndg. Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Kiembesamaki kupitia CCM.

  Kesho mgombea huyu wa CCM atachukua fomu za tume za kugombea. Uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Mohamed Gharib Bilal.
 
Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi.
 
Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili.

  Kamati Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu.
   
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
13/01/2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments