Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Januari 7, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mheshimiwa Youcef Yousfi ambaye yuko katika ziara ya siku sita nchini.
Katika ziara hii, Mheshimiwa Yousfi na ujumbe wake unaojumuisha viongozi wa mashirika ya umma, wanatarajia kutembelea kituo cha umeme cha Gridi ya Taifa cha Ubungo mjini Dar es Salaam, ujenzi wa bomba la gesi katika eneo la Vikindu na Mkuranga mkoani Pwani, machimbo ya Mererani na Minjingu mkoani Manyara.
Rais Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake na ziara hiyo, akisisitiza kwamba Tanzania na Algeria zimekuwa marafiki na washirikia wa karibu wa siku nyingi katika masuala ya siasa na uchumi, kufuatia misingi imara iliyowekwa na waasisi wa nchi hizo - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mheshimiwa Ahmed Ben Bella,
Rais amebainisha kwamba ushirikiano wa nchi hizi mbili ni muhimu sana sio tu katika kuendeleza uhusiano wao wa muda mrefu, bali pia katika uwekezaji na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.
Alisema Rais: "Tunahitaji washirika wazoefu, waaminifu na wenye ujuzi katika sekta ya mafuta na gesi kama Algeria katika kuendeleza sekta hiyo ambayo ni mpya kwetu".
Alitolea mfano wa uzoefu wa miaka mingi wa Algeria katika uchimbaji na usafirishaji wa gesi asilia katika mradi wa bomba la gesi la Maghreb–Europe, unaounganisha machimbo ya gesi ya Hassi R'Mel nchini Algeria, na kusafirisha gesi asilia hadi nchi za Morocco, Hispania na Ureno
"Tanzania itanufaika sana na juzi na uzoefu wa Algeria katika sekta ya gesi hasa katika wakati huu ambapo Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC) limepewa jukumu la kujiendesha kibiashara hivyo linahitaji washirika mahiri", alisema Rais
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
07 Januari, 2014
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments