[wanabidii] KAULI YA WAZIRI KIVULI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA JUU YA MGOGORO NA YANAYOTOKEA KITETO

Wednesday, January 15, 2014
KAULI YA WAZIRI KIVULI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA JUU YA MGOGORO NA MAAFA YANAYOTOKEA KITETO

Kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto, ambao hadi sasa umesababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na umwagaji wa damu, vifo vya watu na uharibifu wa mali ni muhimu sana hatua za haraka zichukuliwe kuzuia maafa zaidi yasiendelee kutokea.

Mgogoro huu wa Kiteto unaonekana kuzidi kuwa mkubwa pamoja na Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa mwaka huu kuchunguza migogoro yote ya wakulima na wafugaji nchi nzima, ikiwa imeshapita katika eneo hilo, ambapo ilitegemewa 
ingeweza kuwa imesaidia kuupunguza au kuumaliza kabisa ili wakulima na wafugaji hao waendelee kuishi na kufanya kazi zao kama ndugu.

Hivyo kupitia Wizara Kivuli ya Kilimo, Chakula na Ushirika, tunataka yafuatayo yafanyike;

Kwanza, Serikali isitishe operesheni yoyote inayoendelea katika eneo hilo lenye mgogoro wa pande mbili, wakulima na wafugaji, kila upande ukidai haki yake.

Ni muhimu kuchukua hatua hiyo kwa sababu, kutokana na tatizo la migogoro kati ya wakulima na wafugaji kuzidi kuwa sugu katika maeneo mbalimbali nchini, hali ambayo imekuwa ikisababisha madhara makubwa kama inavyotokea sasa Kiteto, mwaka huu Bunge limeunda Kamati Teule kwa ajili kuichunguza, kisha itoe taarifa bungeni kwa ajili ya hatua za kibunge.
Kwa wakati huu ambapo bunge linasubiri taarifa hiyo ya Kamati Teule ni vyema Serikali ikasitisha operesheni inazofanya katika eneo hilo, hadi hapo chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi kitakapokuwa kimepokea taarifa hiyo, kuijadili na kutoa maagizo ambayo tunaamini yatatoa suluhu ya kudumu ya migogoro mingi, ukiwemo huu unaoendelea sasa Kiteto.

Pili, kupitia mgogoro huu wa Kiteto ambao umefikia hatua ya kusababisha mauaji ya watu, tunaitaka Serikali hii ya CCM kupitia kwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Christopher Chiza, ijitafakari sana juu ya uwezo wake wa kushughulikia viini vya matatizo kwa uharaka, umakini na usahihi badala ya kuwa mabingwa wa kushughulika na matokeo ya tatizo, wakiwa wamechelewa.

Tatu, kutokana na hayo ambayo yameshatokea Kiteto hadi sasa, ambapo damu za watu zimemwagika katika suala ambalo lilipaswa kuwa limeshapatiwa ufumbuzi kama serikali ingelikuwa inazingatia uwajibikaji kwa wananchi wake, kwa nini Waziri Chiza asiwajibike kujieleza mbele ya umma kuwa Serikali kupitia nafasi yake, imeshindwa na kwamba inahitaji msaada katika jambo hili?

Nne, tunapenda kuishauri Kamati Teule ya Bunge inayoendelea na kazi yake ya kuchunguza migogoro hiyo kufanya kazi hiyo kwa umakini na usahihi ili kubaini kwa uhakika viini vya migogoro husika ili bunge kwa niaba ya wananchi lipate majawabu sahihi yatakayomaliza migogoro hii ili wakulima na wafugaji wapate haki zao kama wananchi wa nchi hii, waendelee kuishi kwa amani na watimize wajibu wao kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Imetolewa leo na;
Rose Kamili Sukum (MB)
Waziri Kivuli wa Kilimo, Chakula na Ushirika

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments