[wanabidii] HONGERA KWA MIAKA 50 YA MAPINDUZI , TULINDE MAPINDUZI

Sunday, January 12, 2014

Na mtaujuwa ukweli na ukweli utawaweka huru. – Biblia Yohane 8:32


Na sema: Ewe Mola wangu! Nipitishe kunako mlango wa ukweli na hishima, na nitowe kupitiya mlango wa ukweli na hishima. Na unipe nguvu kutoka kwako zenye ushindi zinisaidie. – Qur'ani 17:80


Ndugu zangu ,


Napenda kuwapa hongera wale wote waliofanikisha mapinduzi tukufu ya Zanzibar na kuendelea kudumisha mapinduzi hayo mpaka sasa hivi tunapotimiza miaka 50 ya mapinduzi hayo .


Nawapongeza wale wote waliofikiria na hatimaye kufanikisha muungano wa ASP na TANU na hatimaye kuzaliwa CCM na muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo leo tunatamba dunia nzima kama Watanzania .


Katika miaka hii 50 tumepitia mengi , kuna watu wameumia na kuumizwa kwa njia mbalimbali ambazo nia yake ilikuwa ni kuendeleza mapinduzi ambayo leo tunasheherekea miaka hiyo 50 ya mapinduzi tukufu ya Zanzibar .


Basi nichukue fursa hii kuwasisitizia ndugu zangu kusahau yale yaliyopita katika kufanikisha mapinduzi haya na yale yaliyofuatia ambayo ni doa kwa mapinduzi hayo , tuangalie yale mazuri na yanayosaidia kudumisha mapinduzi haya pamoja na mapambano ya kumuinua mwananchi wa Tanzania .


Hongera wanamapinduzi wote .


 Tutaendelea kupigania na kulinda mapinduzi hayo daima na milele .


Tutaendelea kuulinda na kupigania muungano wetu bila hofu , tukiamini muungano utaendelea kuwepo na kudumu milele .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments