[wanabidii] HALI YA KISIASA KWENYE VYAMA VIKUU

Monday, January 27, 2014

Wakati unaposoma makala ya Dr. Kitila, unapata kitu Fulani ambacho ama kilikuwa kimefichika ama kilikuwa kinahisiwa. Kitu hiki ni kugombea madaraka ndani ya chama na baadae katika nchi. Si kosa, maana ndio lengo kuu la chama chochote cha siasa.

Suala hapa ni nani atawahi kupata. Akina Kitila na Zitto walichelewa wakawahiwa kabla ya kufikia lengo lao. Kama alivyosema Kitila, nafasi walizokuwa wakitafuta tayari zina watu ambao hawajawa tayari kuzipoteza! Kila mmoja anafanya awezalo kulinda nafasi yake. Hawa wamewahiwa!!

Binafsi, siwaombi wakate tamaa, lakini wajue waliacha msingi muhimu wa uongozi wa pamoja. Na hili litawatafuna maana hata wakirudi, wenzao watawaangalia kama wasaliti. Kikubwa ni kuamua, kurudi ndani ya chama au kutoka kabisa. Kuna hatari kubwa watakapoamua kuendelea na chama chao. Najaribu kuangalia aina ya intelijensia iliyotumika kukusanya takwimu za tuhuma dhidi ya Zitto; hazinipi chembe yoyote ya usalama endapo watang’ang’ania kubaki. Anyway, labda ni hofu yangu lakini vyovyote iwavyo umakini zaidi utahitajika.

 

Deogratias Luhamba| Technical Officer ES| FHI360| Near Nyahanga Primary School, Nyahanga Area | P.O. Box 1007 Kahama-Tanzania| T: +255 28 2711044, M: +255 754 488 582 |dluhamba@fhi360.org |www.fhi360.org|FHI 360 Facebook

 

Share this :

Related Posts

0 Comments