[wanabidii] HAKI ZAKO UNAPOKAMATWA NA POLISI

Friday, January 10, 2014
POLISI AKIJA KUKUKAMATA FANYA HIVI...... 
JUA HAKI YAKO UNAPOKAMATWA NA POLISI. 
• Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako. 
o Mwulize jina lake
o Mwulize namba yake ya uaskari
• Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
• Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
• Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa. 
o Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
• Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
• Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
• Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake. 
• Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa. 
• Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
• Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
• Iwapo askari polisi ataamua kumpekua mtuhumiwa, mtuhumiwa ana haki ya kumpekua askari polisi KABLA ya kupekuliwa yeye mwenyewe. 
• Pia, askari polisi hawana haki ya kuingia kwenye gari, nyumba au ofisi ya mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni ya kufanya upekuzi, pasi na kuwapo kwa (a) hati ya upekuzi ambayo hutolewa mahakamani, (b) mashahidi wanaotambulika rasmi kisheria, kama vile, mwenyekiti/mjumbe wa serikali ya mtaa au mwenyekiti wa nyumba kumi kumi (iwapo mfumo huo unatumika), au (c) jirani wa mtu anayetuhumiwa.
• Aidha, mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na askari polisi baada ya saa 12.30 jioni au kabla ya saa 12.30 alfajiri, kwa mujibu wa Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Penal Code Act), isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba, kumpekua mtuhumiwa kabla ya saa 12.30 alfajiri au baada ya saa 12.30 jioni kunaweza kuleta madhara kwa askari polisi, mashahidi au watu wengine wowote wale.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments