Na Elias Mhegera
Ndugu yangu Zitto Kabwe, nakusalimia kwa upendo wa hali ya juu, natumaini kwamba utauelewa vizuri ujumbe wangu tena katika mtizamo chanya. Kwa muda wote wa mgogoro wenu sikutaka kusema neno kwa sababu kuu mbili:
1. Kwanza niliamini huo mgogoro unaweza kuzaa kitu kizuri zaidi kwa sababu mara nyingi ni katika migogoro ndipo watu hujifanyia tathmini yao binafsi na kujipima wao wamechangia vipi katika kile kinachoendelea mbele yao. Katika hilo simaanishi kukuhukumu wewe bali pande zote mbili za mgogoro huo.
2. Pili ni kwa sababu sisi au mimi kwa kuwa ni muajiriwa katika asasi ya kiraia siruhusiwi kujihusisha na masuala ya kisiasa ingawaje pia sizuiliwi kutoa maoni yangu kama Mtanzania mwingine.
Kwa bahati mbaya niliishagundua kwamba nikitoa mawazo yangu tayari nitakuwa nimejivua nguo zangu juu ya matamanio yangu kwa nchi yangu Tanzania.
Labda wapo sasa watakaonihukumu kwa kila nitakachokisema kwamba kinatokana na dhamira yangu ya kuona kwamba CCM inaanguka!, la hasha!
Lakini kabla sijasogea mbele labda nikufahamishe kwamba tayari nilishaanza kuamini kwamba Mungu alikuwa ameweka 'upako' katika chama chenu ambacho mimi siyo mwanachama wake lakini kwa nia njema na mapenzi mema kwa nchi yangu kiliishanipa matumaini makubwa!
Nikawa nakumbuka maneno ya Biblia, Luka 12:32 "msiogope enyi kundi dogo! Maana baba yenu amependa kuwapeni ufalme!" lakini kadri siku zinavyosonga mbele naanza kuwa na wasi wasi kwamba shetani sasa anaiharibu kazi yenu takatifu!
Leo Bwana Zitto unazungumzia masuala ya kifo cha Marehemu Chacha Wangwe unataka kutoa taswira gani kwa Watanzania? Kumbuka Watanzania wengi ni waelewa na vifo vya ghafla ni rafiki wa 'usaliti wa ghafla' hiyo ni kanuni!
Labda busara yangu ndogo itoshe kukumbia kwamba katika maisha jaribu kujizuia kuwa na uamuzi wowote wa ghafla sana (u-turn decisions) kwa sababu historia inaonyesha kwamba wengi waliofanya hivyo walikumbwa na dhahama na wengine walipoteza maisha yao.
Kwa hiyo iwapo wewe utapata madhara si lazima sana uwe umefanyiwa na Mhe Freeman Mbowe, Dkt Willibrod Slaa n.k. bali hata wengineo ambao wataona unataka kufifisha matumaini yao kwa huo msimamo wako wa kumwaga hadharani siri za chama kisa? Mgogoro na Mbowe!.
"usiukate mkono ukulishao" huo ndio ujumbe wangu na wala usiyatupe ghafla yale uliyoyasimamia kwa muda mrefu. Nitakupatia mifano michache ya waliokufa katika mazingira yenye utata baada ya kufanya "u-turn decisions" na wala hii si kutishia maisha yako!
Marehemu Samora Machel wa Msumbiji alikufa ghafla katika ajali ya ndege baada ya kusaini mkataba wa Nkomati na makaburu (1984). Anwar Sadat wa Misri alikufa ghafla kwa kupigwa risasi baada ya mkataba wa Camp David na Menachem Begin wa Israel (1979), Yitzhak Rabin aliuawa ghafla kwa risasi baada ya kusaini Mkataba wa Oslo na Yasser Arafat kiongozi wa Wapalestina (1995).
Hata hapa Tanzania ndani ya CCM Prof Kighoma Malima alikufa ghafla (1995) baada ya kuhama kutoka CCM na kujiunga NRA kisha kuibadilisha kuwa NAREA baada ya kuvuliwa uwaziri wa fedha. Vivyo hivyo Horace Kolimba alikufa ghafla baada ya kuvuliwa ukatibu mkuu wa CCM na kisha baadaye akasema chama hicho kimepoteza dira na mwelekeo!.
Kila la kheri ndugu yangu!
mhegeraelias@yahoo.com simu: 0754826272
-- Ndugu yangu Zitto Kabwe, nakusalimia kwa upendo wa hali ya juu, natumaini kwamba utauelewa vizuri ujumbe wangu tena katika mtizamo chanya. Kwa muda wote wa mgogoro wenu sikutaka kusema neno kwa sababu kuu mbili:

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments