TANZANIA IMEJIPANGAJE KATIKA KUKABILIANA NA UDUKUZI ?
UDUKUZI NI NINI ?
Ni uchukuaji wa taarifa za mwingine kwa njia ambazo sio halali kwa kutumia vyombo vya mawasiliano anavyotumia mtu husika kama email , simu , kompyuta , tv na vingine vingi .
Taarifa hizi zinaweza kuwa kwa njia ya nyaraka zilizohifadhiwa , zinazofanyiwa kazi ( kama ziko shared ) , kusikiliza mawasiliano ya sauti kama kupiga au kupokea simu , ujumbe mfupi yaani sms na Mawasiliano ya email mtu anayofanya na watu wake au makundi .
Katika siku za karibuni wigo umepanuka kidogo sasa hivi mpaka kwenye anuani za watu kwenye mitandao ya kijamii kama facebook watu wanaouwezo wa kuiba taarifa au kuingia na kupotosha , kwenye majukwaa ya majadiliano pia watu wanaweza kuingia kuvuruga au kuiba taarifa za mtumiaji fulani bila wenye jukwaa kujua .
Kwa mataifa yaliyoendelea Aina hii ya Ujasusi ni njia moja wapo ya kujilinda dhidi ya adui wa nje na wa ndani , adui huyo anaweza kuwa gaidi , jasusi mwenzake , biashara za kimataifa , teknologia , uuzaji na usambazi wa silaha , taarifa za afya , viwanda na nyingine nyingi .
MATUKIO MAARUFU YA UDUKUZI KIMATAIFA
1 – Miezi kadhaa iliyopita tumesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kuhusu Udukuzi uliokuwa unafanywa dhidi ya viongozi mbalimbali wa nchi za ulaya na amerika ya kusini na mashirika ya ujasusi ya kimarekani .
2 – siku kadhaa kabla ya mkutano wa G20 NA hata wakati mkutano huo unaendelea baadhi ya wajumbe walipokea barua pepe ambazo zilikuwa na program maalumu zilizojiingiza kwenye kompyuta zao na hapo hapo walianza kufuatiliwa na kuibiwa taarifa zao haswa kile walichokuwa wanafanya na kuandika kutumia kompyuta zao na simu , uchunguzi ulipofanyika iligundulika uvamizi huu ulitokea uchina .
3 – wajumbe wa mpango wa nyuklia wa irani walipoenda uingereza kwa ajili ya mkutano Fulani nao waliingiziwa virusi walipowasha tu vifaa vyao vya mawasiliano , virusi hivi vilisambaa mpaka kwao mpaka kwenye vinu vyao vya nyuklia matokeo yake ni kwa baadhi ya vitu kutokufanya kazi sawasawa .
Hili suala kwa Irani pamoja na vikwazo ndio limesababisha uongozi mpya kutaka muafaka na mataifa yaliyoendelea , pia lilisababisha baadhi ya wanasayansi wao kuuwawa kwa njia za kigaidi haswa wale waliokuwepo kwenye mradi huu .
MATUKIO MAARUFU YA UDUKUZI NCHINI
Kwa hapa nchini kuna matukio 3 ambayo ni maarufu lakini hayajawahi kuongelewa sana .
1 – Waziri mmoja na kundi lake walikuwa wanaenda nchi Fulani ya ulaya kwa ajili ya warsha na alitarajiwa kutoa msimamo Fulani , basi alivyofika hotelini kuwasha kompyuta yake kuanza kupekua vitu hapo maharamia wa mtandao walimvamia na kuharibu hiyo kitu aliyokuwa anafanyia kazi siku zote .
2 – Mara kadhaa kumewahi kutokea udukuzi kwenye taasisi zetu zinazosimamia maswala ya mawasiliano haswa TCRA na ilipochunguzwa ikagundulika waingiliaji wengi walitokea nchi ya China , china imekuwa nchi inayongaa ulimwenguni kwenye masuala ya Udukuzi .
3 – Udukuzi uliwahi kufanywa dhidi ya shirika moja la ndege nchini halafu wahalifu wakavamia kwa nia ya kuharibu utaratibu wa urushaji ndege na uhifadhi mwingine wa taarifa , hii ilisababisha ndege moja kukaa uwanjani bila kufanya safari kwa mwezi mmoja kwa sababu za kiusalama na ndege hiyo ilikuwa inaendeshwa na mitambo maalumu kutoka nchi nyingine .
HALI YA TANZANIA
Hali ya Tanzania kusema za ukweli sio ya kuridhisha sana kutokana na mambo 3 makuu .
1 – Sheria za Mawasiliano – Sheria zetu za mawasiliano hazijitoshelezi na wahalifu wengi wanatumia fursa hiyo kufanya uhalifu wao kutoka hapa kupiga wengine au kupitia hapa kupiga wengine wa mbali , tunapenda kuwa na sheria nzuri za mawasiliano zinazoendana na wakati wa sasa na kila idara serikalini itengeneze sheria zake kwa kunukuu sheria mama .
2 – Utumiaji wa Vifaa chakavu – Tunaona watu haswa wenye fedha zao wakinunua vifaa chakavu vya mawasiliano haswa toka nchi za mbali kwa ajili ya kuja kutumia hapa nchini vifaa hivi vingi vimesababisha utengenezwaji wa njia za kivamizi na kwa sababu teknologia zake za kizamani imekuwa rahisi wa wahalifu kuzichezea na kufanya wanachojua .
3 – Vifaa visivyokidhi viwango – Tumeona watu wananunua simu ambazo hazina viwango na kuzitumia kwenye shuguli za uhalifu , simu nyingine zinapunguzwa baadhi ya vitu ili ziweze kufanya kazi nchini , watu maofisini wanaingiza programu kwenye kompyuta zao ambazo hazina leseni au leseni bandia yote hii haitakiwi .
4 – Kutokufuata taratibu za manunuzi – Hapo juu nimesema hatuna sheria za mawsiliano na tumezoea kununua vifaa chakavu , tukiwa na hivyo viwili tutaweza kuwa na utaratibu mzuri wa kununua vifaa haswa vya mawasiliano maofisini na kwenye idara za serikali utakaofuata vitu hivyo viwili .
NINI KIFANYIKE
Ni wakati mzuri sasa kwa Taasisi muhimu nchini kama Mabenki , Polisi , Tume ya mawasiliano , Kampuni za Mawasiliano ya Simu na Intaneti , taasisi za elimu kama vyuo na shule kuwa na taratibu za kufundisha watu matumizi salama ya vifaa vya mawasiliano , ununuzi mzuri wa vifaa vya mawasiliano na uuzaji mzuri wa vifaa vya mawasiliano .
Tufanye hivi huku tukingoja sheria mama wa mawasiliano iboreshwe na wengi wataboresha masomo yao kuzingatia sheria mama ya mawasiliano nchini kulingana na hali tuliyonayo .
Ningependa kuona sheria mama ikiandikwa kutokana na mila na tamaduni za mtanzania sio nje ya hapo , hata pale mtu akisoma itoe harufu ya utanzania au uafrika mashariki .
Kupambana na udukuzi wote sio rahisi lakini tunaweza kupunguza uwezo wa kufanyiwa udukuzi kwa kuhakikisha tuna vifaa vizuri vya mawasiliano na kufuata taratibu za utumiaji .
YONA FARES MARO
0786 806028
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments