TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MWALIKO KWA MAKUNDI MBALIMBALI KUPENDEKEZA MAJINA YA WATAKAOTEULIWA KUWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
MWALIKO KWA MAKUNDI MBALIMBALI KUPENDEKEZA MAJINA YA WATAKAOTEULIWA KUWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anapenda kutoa mwaliko kwa makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwasilisha orodha ya watu wasiopungua wanne na waziozidi tisa kwa ajili ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2A) cha kifungu cha 22 cha sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sura ya 83 kinachomtaka Rais kuwaalika kila kundi lililoainishwa chini ya kifungu kidogo cha (1) (c) kutoka pande zote za Muungano kuwasilisha kwake orodha ya majina yasiyopungua 4 na yasiozidi 9 kwa ajili ya kuzingatiwa katika uteuzi.
Makundi hayo ni kama ifuatavyo:
1. Taasisi zisizokuwa za Kiserikali
2. Taasisi za kidini
3. Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
4. Taasisi za elimu ya juu
5. Makundi yenye ulemavu
6. Vyama vya wafanyakazi
7. Vyama vinavyowakilisha wafugaji
8. Vyama vya wakulima
9. Vyama vinavyowakilisha wavuvi
10. Makundi mengine yenye malengo yanayofanana
Katika kuwasilisha majina hayo, makundi yaliyoalikwa yatalazimika kuonesha umri, jinsia, uzoefu, sifa na sehemu ya makazi ya mtu aliyependekezwa ikiwa ni pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia.
Mheshimiwa Rais ameelekeza kuwa orodha ya majina yanayopendekezwa yawasilishwe kwa maandishi ama kwa kupeleka kwa mkono au kutumia huduma ya posta kwa anuani zifuatazo:
1. Katibu Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais, Ikulu,
S.L.P. 9120,
DAR ES SALAAM
2. Katibu Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais,
S.L.P. 4224,
ZANZIBAR
Mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo ni tarehe 02 Januari, 2014.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments