Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO), Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa.
Katika uteuzi huo, Rais amemteua Prof. Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine
Katika uteuzi huo, Rais amemteua Prof. Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO).
Rais pia amemteua Bwana Freddy Safiel Manongi kuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ambaye hivi sasa ni kaimu Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori cha Mweka na pia amemteua Prof. Audax Zephania Philip Mabula kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa.
Uteuzi huu umeanza rasmi mwishoni mwa Mwezi Oktoba mwaka huu.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments