[wanabidii] POLISI JIJINI MWANZA LAFANYA JARIBIO LA KUKABILIANA NA MAGAIDI

Thursday, November 07, 2013
Ikiwa ni mwezi mmoja na siku kadhaa zimepita tangu kutokea kwa tukio la kigaidi la uvamizi wa maduka ya Westgate mjini Nairobi yaliyofanywa na kundi la wanamgambo wa al-Shabaab, asubuhi ya leo ya Novemba 7 2013, mamlaka za usalama Mkoani Mwanza zimefanya uvamizi kwenye hoteli ya Gold Crest ya jijini Mwanza.
Uvamizi huo ambao kwa taarifa za awali kutoka katika vyanzo vyetu lilikuwa ni la jaribio kuona uwezo na namna ya wananchi na jamii kwa ujumla wanavyoweza kukabiliana na matukio ya aina hiyo.
Hata hivyo tukio hilo lililochukua muda wa saa nzima limeibua takaruki kwa wananchi waliokuwa ndani ya hoteli na nje ya hoteli hiyo jambo lililopelekea umati wa watu wengi kukusanyika kwa lengo la kujua nini kinachoendelea.
Hakika kwa utamaduni huu wa watanzania kukimbilia kwenye eneo la tukio badala ya kukimbia sehemu salama kuna hatari ya watu wengi kupoteza maisha kama tukio kama hili likitokea katika mazingira ya uhalisia (tunaomba manani atuepushe na mabalaa ya namna hii). Tazama picha zote za tukio hili lakini nitoe angaliazo tu kuwa TUKIO HILI NI LA MAJARIBIO NA LIMEFANYWA KWA KUSHTUKIZA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments