MIONGOZO YA UTENDAJI KWA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII.
Utangulizi.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii imeundwa kwa sheria Na. 8 ya 2008 ,kama ilivyorekebishwa na Sheria Na.5 ya mwaka 2012, Jukumu kuu likiwa ni Kusimamia na Kuboresha utendaji wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini.
Vilevile Mamlaka inajukumu la kulinda, kutetea na kuendeleza maslahi ya wanachama wa sekta ya Hifadhi ya Jamii. Kwa kuzingatia haya, Mamlaka imetoa miongozo sita ambayo yote inalenga katika kuhakikisha kuwa sekta ya hifadhi ya jamii inakuwa bora na endelevu na hivyo kuboresha maisha ya wanachama na kuchangia maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Miongozo iliyotolewa na mamlaka ni kama ifuatavyo;
I. Miongozo ya Uandikishaji wa wanachama.
Miongozo hii inalenga yafuatayo;
• Kuongoza Bodi za Mifuko ya hifadhi ya jamii kufanya usajili wa wanachama kwa mujibu wa sheria;
• Kuhakikisha kwamba mwanachama mpya anapata haki yake ya kuchagua Mfuko wa Hifadhi ya Jamii anaopenda kujiunga nao;
• Kuondoa migongano kati ya Mifuko wakati wa uandikishaji wanachama wapya;
• Kuainisha taratibu kwa mwanachama wa Mfuko wa hiari kuhamia Mfuko wa lazima;
• Kuongeza wigo wa wanachama katika sekta ya hifadhi ya jamii
II. Miongozo ya Uwekezaji.
Miongozo hii inalenga yafuatayo;
• Kuelekeza Bodi za Mifuko kufanya maamuzi ya uwekezaji kwa mujibu wa sheria.
• Kuhakikisha uwekezaji wa Mifuko unaleta maendeleo bila kuhatarisha afya ya Mifuko, pamoja na kuhakikisha uwekezaji unafanywa kwenye maeneo yenye tija, kukuza uchumi wa nchi na kuboresha mafao ya wanachama.
• Kuhakikisha kwamba Mifuko muda wote inaweza kulipa wanachama wanaostahili mafao
• Kuhakikisha kuwa utawala bora unazingatiwa katika shughuli zote za uwekezaji.
• Kuhakikisha kuwa wanachama wananufaika na uwekezaji unaofanywa na Mifuko
III. Miongozo ya Takwimu
Miongozo hii inalenga yafuatayo;
• Kuainisha kumbukumbu ambazo ni lazima zitunzwe na Mifuko;
• Kuelekeza mifumo ya kuandaa na kuweka taarifa za Mifuko;
• Kuelekeza taratibu za kutoa taarifa za wanachama na michango yao;
• Kuelekeza taratibu za kuhahikisha kwamba taarifa za Mifuko zinapatikana muda wowote zinapohitajika.
IV. Miongozo ya Utawala bora wa bodi za Wadhamini.
Miongozo hii inalenga yafuatayo;
• Kukuza utawala bora katika bodi za Mifuko;
• Kanuni za Mifuko kuzingatia vigezo vya utawala bora katika uendeshaji wake;
• Kuwaongoza wadhamini kutimiza wajibu wao kisheria;
• Kuweka sifa na masharti ya mtu kuwa mjumbe wa Bodi ya Mfuko;
• Kuweka viwango vya taratibu na miundo vya kukuza utawala bora;
• Kukuza na kuendeleza imani ya umma kwa Mifuko
V. Miongozo ya Tathmini za Mifuko.
Miongozo hii inalenga yafuatayo:
• Kuweka taratibu za namna ya kufanya tathmini za mifuko;
• Kuweka vigezo vya kuzingatia kwa makampuni na wataalum wanaotarajia kufanya tathmini za mifuko;
• Kufanikisha kupata taarifa ya tathmini inayoeleweka na yenye taarifa sahihi.
VI. Miongozo ya Kujumlisha vipindi.
Miongozo hii inalenga yafuatayo:
• Kuainisha taratibu za kujumlisha vipindi vya michango kwa wanachama waliochangia katika Mifuko zaidi ya mmoja;
• Kuainisha masharti ya kuunganisha vipindi;
• Kumsaidia mwanachama aliyechangia Mfuko zaidi ya mmoja kupata haki yake stahiki.
Mwelekeo wa Mamlaka;
Ni mategemeo ya Mamlaka kuwa katika kipindi cha miaka 5 ijayo;
• Sekta itakuwa endelevu na kukua;
• Kutakuwa na idadi kubwa ya mifuko ya ziada ya Hifadhi ya Jamii;
• Mifuko itakuwa na mafao bora zaidi na endelevu;
• Ukuaji wa Mifuko ya hifadhi ya Jamii na mahusiano na mamlaka zinginezo za sekta ya hifadhi ya Jamii.
-- Utangulizi.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments