[wanabidii] MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WATANZANIA NCHINI KENYA

Monday, November 25, 2013

MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WATANZANIA NCHINI KENYA


Ndugu zangu ,


Kumekuwa na matukio ya kutisha dhidi ya raia wa watanzania wanaosoma , kuishi Kenya au kwenda tu kwa ajili ya safari zao mbalimbali za kikazi nchini humo matukio haya ni ya kutisha kama sio ya kuogofya na ukizingatia hali ilivyo afrika mashariki kwa sasa ya usalama ndio matukio haya yanaongezeka .


Binafsi niliwahi kupoteza ndugu yangu miaka 3 iliyopita kule Mombasa , huyu ndugu yangu alikuwa anaishi huko na wazazi wake kwenye biashara ya mahoteli basi wakamvizia usiku wakaenda wakanyonga mpaka leo kesi yake haijulikani ilivyoisha isha .


Wiki iliyopita kuna mtanzania ameuwawa kinyama alipokuwa anatoka kwenye ukumbi wa disko , kutokana na maelezo ya awali wanasema alishawasiliana na rafiki zake kwamba ndio anatoka ukumbini kurudi nyumbani lakini hakufika mpaka alipokuja kuokotwa akiwa ameshafariki dunia .


Weekend hii ya kuamkia leo kuna mtanzania amepatikana hospitali Fulani huko jijini Nairobi akiwa hajitambui kabisa ikagundulika ni daktari na mfanyakazi wa wizara ya afya huko Zanzibar mpaka naandika hivi mkewe ameshaenda huko lakini hajitambui inaonekana walimpiga na kitu kizito usoni upande wa jicho .Hatujui baada ya uhalifu huu wamemwibia taarifa gani au nini .


Inaonyesha watanzania wamekuwa target ya uhalifu wa kikenya haswa jijini Nairobi na Mombasa na muda wote huko serikali yetu kupitia balozi wetu huko Kenya hajawahi kutoa tamko lolote wala chochote hata hii habari ya huyu daktari pia watu wako kimya sijui wanataka sasa watu wafanye nini ? wajilinde wenyewe ?


Hali hii inanikumbusha kipindi Fulani wakati wa machafuko ya kibaguzi huko afrika kusini dhidi ya watu wasiokuwa raia wa afrika kusini , siku moja makundi ya vijana wa afrika kusini walikuwa wanaenda kuvamia kwenye sehemu walizokuwa wanakaa raia wa afrika magharibi haswa naigeria hawa jamaa wa naigeria walikuwa wamejiandaa na silaha zao bastoli , bunduki na nyingine mbalimbali wakawa wanawangoja hawa vijana wa zuma .


Wale vijana wa zuma kuona vile na jeshi la polisi kuona vile ndio mzozo ukaishia hapo .


Tusingependa itokee hivi kwa ndugu zetu na jirani zetu hapo Kenya pale ambapo watanzania watachoka kuumizwa na kuuwawa kwa kunyongwa kila mara .


Naomba serikali kupitia waziri mhusika wa mambo ya nje au wa afrika mashariki na balozi wetu hapo Kenya watoe tamko la kuhusu kile kinachoendelea huko Kenya na kuhakikishia watanzania hao usalama wao huko Kenya .


--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments