[wanabidii] CHADEMA YATIMUA MWENYEKITI WA BAVICHA MKOA WA MBEYA

Friday, November 15, 2013
Bundi wa fukuza ili tusinde uchaguzi wa ndani ametua tena mbeya ndani ya chama cha chadema baada ya kamati tendaji ya wilaya hiyo (chadema) kuamua kuunda tuhuma ili kuwafukuza watu wote ambao ni tishio kwa uchaguzi hasa kwa kambi ya mwenyekiti wa wilaya ambaye anawania tena kushinda uchaguzi huo. Hata hivyo mwenyekiti huyo amekuwa akiandamwa na tuhuma lukuki ikiwemo ya kula fedha kutoka chama cha mapinduzi kwa ahadi ya kuhakikisha sugu anashindwa uchaguzi ujao kwenye kura za maoni na yeye kufadhiliwa na ccm ili akagombee ubunge jimbo la rungwe magharibi katika kufanikisha hilo amekuwa akitaka kuwa fukuza watu wote wanapinga mpango huo wa kumwangusha sugu na kumweka mtu ambaye ni mnyakyusa kwa madai kuwa sasa ni zamu ya wanyakyusa kushinda mbeya mjini maana mbunge wa mwisho mnyakyusa mbeya mjini alikuwa mwaiseje wa nccr mageuzi 1995 katika mpango huo unaendeshwa kwa siri sana inadaiwa kuwa hatua za awali ni kuhakikisha vyama vya ccm na chadema vinaweka wagombea wanyakyusa na kinacho mponza joseph mbilinyi ni kabila analotoka (mkinga) ushahidi tayari upo wa mpango huu na muda si mrefu utakuwa wazi.katika risti hiyo ya wanaofukuzwa ni kuwa wafukuzwa halisi ni kumi na nne ila wengine watatu kwa marengo maalum ya kupeleleza kinachoendelea miongoni mwao hii ni kwa mjibu wa chanzo chetu cha habari ndani kikao hicho cha kamati tendaji ya chama hicho mbeya mjini chanzo hicho kinasema kuwa chenyewe hakiridhiki na mpango wa kumwondoa sugu ila kinaunga mkono watu hao kufukuzwa kwa madai kuwa wamekuwa wasumbufu mno kwa kufuatilia kila kitu kinachofanywa na viongozi wa wilaya hata masuala binafsi kama vile uhusiano nje ya ndoa ambao unawaanda ma viongozi hao wa chadema mbeya mjini inasemekana mwenyekiti huyo wa chadema mbeya mjini aligawa viti maalum kwa madem zake na kuwanyima viti hivyo wote waligoma kutoa rushwa ya ngono kinasema chanzo chetu hicho cha habari alipoulizwa watawafukuza kwa sababu zipi alisema watasema wamekura fedha za mhe.lowasa na tunajua hii watashinda lakini itakuwa uchaguzi wa ndani umepita na hivyo watakuwa nje ya chama. Cha ajabu zaidi alipoulizwa kama je chadema taifa wakibadili uamuzi itakuwaje? Alicheka sana na kusema mbowe hana lolote mbele ya mwambigija na mwambigija aliahidi kuwa atawafukuza wote wenye kelele .mwisho orodha ya wanachama hao waliofukuzwa ni kama ifuatavyo.............1.joseph kasamba (m/kiti bavicha mkoa) 2.mwalwiba (alikuwa kampeni meneja wa mbunge sugu 2010) 3.amina mkakile( rafiki mkubwa wa sugu) 4. God mbwile 5. Xb 6.sorwa 7.kelvin 8.zuberi mwasasu 9.gideon mwanjoka 10 geofrey sanga 11. Mzee mkusa 12.hugho kimalio 13.ester silipa 14.jeni jojo 15 cosmas sanga (katibu bavicha mbeya mjini) 16.moses mwakasaga. Kwa mjibu wa mjumbe mmoja wa kamati tendaji ambaye ni mfanyabiashara katika soko moja jijini humo ni muuza mazao anasema watu hawa hatuwapi barua ila uchaguzi ukianza siku hiyohiyo ndo tunawapa barua hizi ili wachelewe kukata rufaa. Hata hivyo watu hao wameapa kuwa watawapeleka mahakamani wajumbe wote wa katai tendaji kama watakosa ushahidi wa kuonyesha ni namna gani waliweza kuchukua au kuhongwa fedha na mh. Lowasa wanasema hawatashitaki chama wanakiheshimu watashitaki viongozi wanaowazushi mambo kila uchao na kusimamisha uchaguzi kwa njia ya mahakama mpaka suala lao liishe mwisho wa sinema ya kweli toka jijini mbeya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments