Hili swala naomba tulijadili kizalendo na tutangulize maslahi ya taifa mbele.
Binafsi ninakerwa na jinsi serikali anavyotegemea kodi kwenye mambo yaleyale ya kila siku. Walipa kodi wasio na shaka Tanzania ni Wafanyakazi wa Umma,wakati kipato chao ni kidogo kisichotosheleza hata kwa matumizi ya wiki mbili.
Wafanya biashara wengi karibu 70%hawalipi kodi huku wakizalisha na kujitajirisha kila kikicha. Kama kuna kazi ambayo inaongoza kwa kulipa basi biashara inaongoza. lkn chakushangaza ni kuwa wafanyabiashara wa Tanzania hawalipi kodi ipasavyo na badala yake wamekuwa mabingwa wa propaganda na vitisho kwa serikali ili waendelee kufanya kazi bila kulipa kodi.
Mbinu chafu zinazofanywa na wafanya biashara wa tanzania bila kificho ni kama ifuatavyo.
Mteja unaponunua bidhaa huandikiwa receipt kwenye kijitabu cha receipt ambacho baadae hukaguliwa na TRA ili kufanya mahesabu. wanachofanya ni kuwa ikinunua bidhaa za laki tano wao hukuandikia shilingi elfu hamsini na baada ya kuandika,risiti huchanwa na nakala hubaki kwenye kijitabu cha risiti,anapoichana risiti kwaajilo ya mteja huiongea sifuri ili isomeke laki tano.wakati kwenye kitabu inasomeka elfu hamsini.hebu jiulize kwa mchezo huu mfanya biashara amekwepa kodi kiasi gani? hili nalo tulishangilie? au tushirikiane kuwahimiza wafanya biashara walipe kodi ili taifa letu lisonge mbele?
Kesi za kuchakachua risiti nimeziona mwenyewe tena ktk maduka tofauti na kwa wakati tofauti tofauti.haya yanafanyika zaidi mikoani sina hakika sana na Dar es Salaam,lkn zaidi ya mikoa sita niliyofanikiwa kufika na kununua bidhaa utaratibu wao ni huo. Mikoa ya Tanga,Kigoma,Tabora,Singida na Morogoro huo ndio utamaduni wao.
Njia ya pili ya kukwepa kodi kunakofanywa na wafanya biashara wa kada ya kati, ni kuwa unaponunua bidhaa unapewa risiti halali kabisa(manual riceipt) hii ni kwaajili ya kumlinda mteja ili mzigo usikamatwe na maofisa wa TRA ,pindi mzigo unapofika unakokwenda,mathalani kutoka duka la jumla kwenda maduka ya mitaani,mzigo unapofika mteja hutakiwa kurejesha risiti kwa mteja wake wa duka la jumla.na anapo rejesha risiti kwa aliemuuzi risiti hiyo hukatwa(being counceled) na kuonekana kuwa risiti olikuwa imeshaandikwa lkn bidhaa hazikutoka.hivyo biashara iliahirishwa na hivyo risiti iliyositishwa huambatanishwa kwenye kijitabu cha risiti na hivyo siku ya mahesabu risiti hizo hazitahesabiwa. Hili nalo tuendelee kuwapongeza wafanya biashara na kuwaona mashujaa dhidi ya serikali?
Tuongozwe na uzalendo wa kweli,katika kulijadili hili kwa maslahi mapana ya Taifa,na si itikadi za vyama vyetu vya siasa.
TRA kuamua kutumia mashine za kielektroniki kutolea risiti kwa wateja ni njia ambayo kama taifa ingetusogeza mahala flani. Lkn kwa wafanya biashara waliozoea kufanya biashara bila kulipa kodi stahiki ni mwiba mkali tena usiovumilika, mfanya biashara siku zote nawaza kupata gaida kubwa(maximazation of profit) njia hii itawaganya wafanyabiashara watoe kodi stahiki kwakuwa taarifa za kmteja huhifadhiwa katika data base na hivyo hawana pa kutokea zaidi ya kuzikataa machine kwa propaganda ya kuwa zinauzwa laki nane hivyo bei ni kubwa.lengo ni kutaka kuendeza utamaduni wao wa kutoa risiti za mkono .
Mwalimu mwenye mshahara wa 263000/= analipa kodi ya sh.34190/= mwezi. Mwalimu mwenyeshahada analipwa ujira wa takriban 532000/= na kodi anayolipa mtu huyu ni karibu 69160/=kwa mwezi, mwalimu huyu analipa karibu 829920/=kwa mwaka pesa ambayo ni zaidi ya gharama ya hiyo mashine inayolalamikiwa ma wakwepa kodi wakongwe. Hatuwezi kuwa na Taifa linalojengwa na kundi dogo la wafanyakazi pekee licha ya kuwa wanakipato duni ukilinganisha na wafanyabiashara.
Tumechoka kuona watu wasiolijenga taifa wakiwa wanashangiliwa na wananchi bila kutafakari mustakabali wa taifa.
Pamoja na yote niliyoandika hapo juu maafisa wa TRA nao wamekuwa ni sehemu ya tatizo kwa kuendelea kulea upuuzi na kushirikiana na wafanya biashara wasio waaminifu.Mfano wapo wafanyabiasha wasiolipa kodi kwa makusudi kwa kiburi cha kushirikiana na baadhi ya maafisa wa TRA .Baadhi ya Maafisa wa TRA anamaduka ambayo hayalipi kodi na badala yake wanamalizana juu kwa juu,yupo Mfanya biashara maarufu jijini Dar es Salaam ambae ni mwingizaji wa bidhaa toka nje kupitia bandari ya Dar es Salaam,anapoingizi kontena 10 analipia nusu ya mzigo na nusu nyingine humalizana na baadhi vigogo wa TRA na hivyo Taifa kukosa pesa ambazo zingetusaidiaa kutuletea maisha bora kwa kila mtanzania.
Mwisho nimalize kwa kuwaomba watanzania wote kwa umoja wetu,kuwapinga wote wasiotaka kulipa kodi .pia serikali inapaswa kutimiza wajibu wake na kuwafukuza watendaji wabovu wasiotimiza wajibu wao.
Tuige mfano wa china ambapo kila raia hudai risiti pindi anaponunu bidhaa yoyote hataa kama ni mboga za majani,tuige nchi zilizoendelea ambazo ambazo mabango na matangazo mengi kwenye vyombo vya habari vinahimiza kulipa kodi. watanzania tuhimizane umuhimu wa kudai risti pindi tunaponunua bidhaa.
Jashia khamisi maarufu.
0714276818
jashiahamisi@gmail.com
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments