[wanabidii] KUSAMEHE KWA HEKIMA NI NINI?

Wednesday, September 11, 2013
KUSAMEHE KWA HEKIMA NI NINI? 

BINADAMU KUNA KIPINDI TUNAKWAZIKA SANA KIASI CHA KUTAMANI KUWAADABISHA WALE WALIOTUKWAZA. LAKINI JE, TUNATAMBUA MADHARA YA HASIRA ZETU ZITOKANAZO NA KUONA KUWA TUMEONEWA, TUMEDHALILISHWA, TUMEDHULUMIWA, TUMEDANGANYWA, TUMESALITIWA NA KADHALIKA? 

Katika hali ya kawaida kusamehe kunaweza kuelezewa kuwa ni hali ya kupuuzia makosa ya mtu fulani au kuachilia/kutupilia mbali madonda ya kihisia ambayo yalisababishwa aidha kwa makusudi ama kwa bahati mbaya. Tatizo la kusamehe kwa kawaida pasipo hekima/umakini ni kuwa wahusika wanaweza kuishia juu juu ya tatizo pasipo kuzama kwenye kiini, ili kubainisha chanzo halisi cha changamoto ama mgogoro. Hatari ya 
kusamehe kwa namna hii ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kosa lile lile kujirudia na hivyo kuukwaza zaidi upande wa pili kufikia kiwango cha kutonesha kidonda kinachopona na katika hali hiyo unaweza kufikiri ni madhara gani yanayoweza kutokea.

Baada ya kusema hivyo ningependa kurejea katika kusamehe kwa hekima ambapo mhusika anayewiwa kusamehe hufanya kila jitihada kuainisha vyanzo vikuu vya kutokuelewana ama visababishi mbalimbali vya kosa husika. Ni kwa kujua chanzo halisi ambapo kusamehe kunaweza kuleta maana kwa kuwa vile visababishi vya choko choko vinadhibitiwa kama siyo kutokomezwa kabisa.

Mtu mwenye hekima ya kusamehe, huelewa kuwa kwa kuwa sisi sote ni binadamu, kwa namna moja ama nyingine sote huwa tunafanya makosa (tunakosea kwa kuwa sisi si wakamilifu), na hivyo mahusiano yetu ya kudumu ni zao la kuvumiliana (kusatahimili mapungufu ya kila mmoja wetu). Ufahamu huu humfanya mwenye kusamehe kuutazama upande wa pili na mtazamo huru (akili huru) yenye utayari wa kupima na kuzingatia mawazo ama maombi ya msamaha ya upande wenye makosa.

Kumbuka: Kabla ya kusamehe ni vema utafakari na hata kufanya juhudi za kubainisha mambo yanayoweza kuwa yamepelekea makosa husika, vinginevyo itakuwa kama kuchemsha chungu kitupu huku ukisubiria supu!

---Dr. Benjamin Najimu Mohamed, 10/9/13, 9: 00PM.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments