Ushauri wa Kuepukana na Msongamano Mkubwa wa Magari na Ajali Nyingi Zinazotokea Katika Barabara ya Sam Nujoma kwenye Mzunguko (Roundabout) ulioko Mlimani City karibu na Kituo cha Mafuta cha Total
Serikali ilifanya kazi kubwa na nzuri ya kujenga barabara ya Sam Mujuma kutoka Ubungo hadi Mwenge ambayo imeboresha sana hali ya barabara hii. Hata hivyo, kama ambavyo wengi watakua wameona, kuna mambo mawili ambayo yanahitaji kuangaliwa upya na kurekebishwa katika barabara hii.
1. Tatizo la Mzunguko (Roundabout) wa Mlimani City kwenye Kituo cha Mafuta cha Total
a. Mzunguko (Roundabout) ulioko eneo la Mlimani City, nadhani ulijengwa kwa makosa kidogo. Sheria ya barabarani inamuhitaji anayekuja kwenye mzunguko apunguze mwendo na kungoja walio ndani ya mzunguko (kulia) kupita kwanza. Alama za kuingia kwenye mzunguko ziko sahihi na zinamtaka anayetokea Mwenge au Ubungo apunguze mwendo anapokaribia mzunguko huu.
b. Pamoja na ukweli huu, mzunguko huu umekua sababu kubwa ya ajali nyingi sana nadhani kuliko eneo lingine lolote katika barabara hii. Kwa kua ninaishi karibu na mzunguko huu na ninapita karibu kila siku ninapokwenda na kutoka kazini au katika shughuli nyingine za kijamii, kwa miaka kadhaa sasa tangu barabara hii ikamilike, nimeshuhudia ajali za kila aina na watu wengi kuumia.
c. Kwa analysis yangu, nimegundua pamoja na kuwa kuna sheria inayoongoza jinsi ya kupita kwenye mzunguko, lakini mzunguko huu ulijengwa kwa makosa. Eneo la katikati la mzunguko huu, ni dogo sana na halijasibabisha tumbo la kutosha la kulazimisha mtu anayekuja kupunguza mwendo anapoingia kwenye mzunguko. Matokeo yake ni kuwa mtu anayetokea Mwenge au Ubungo ana uwezo wa kupitiliza na mwendokasi wowote ule aliokuja nao kwani tumbo la mzunguko ni kama haliko. Iwapo mtu anayekua ndani ya mzunguko akijiaminisha kuwa anayekuja anajua taratibu na akaendelea kupita maana yuko sahihi, anajiweka kwenye hatari kubwa sana. Ni ukweli kuwa wapo madereva wengi sana wazembe na wasiojali sheria na pia wako wengi sana wanaoendesha magari lakini hawajajifunza kabisa sheria za barabarini na hawajui hata nini chahitajika unapokaribia mzunguko. Mara kadhaa nimeshangaa kuona mtu anayekuja kwenye mzunguko akitukana walio ndani ya mzunguko wanaolazimisha kupita kwanza akiwaona ndio wenye makosa.
d. Kwa kifupi ni kuwa kupita kwenye mzunguko huu ni hatari sana na inalazimisha mtu kuwa makini sana hasa pale unapotazama kushoto na kulia na kuona malori, pikipiki na magari menigne yakija na mwendo kasi na hayana mpango wa kupunguza.
Ushauri wangu kama suluhisho kwa tatizo hili
a. Kwa kuwa barabara hii iko chini ya TANROAD, nashauri kuwa kipande hiki cha barabara kijengwe upya ili kuwezesha mzunguko huu umlazimishe anayeingia kwenye mzunguko apunguze mwendo na kungoja walio ndani wapite kwanza.
b. Pamoja na ukweli kuwa ni wajibu wa wanaoendesha vyombo vya usafiri kujua sheria, lakini huenda kazi ya kuhakikisha kila mmoja anafuata sheria isiwe rahisi sana na ikagharimu fedha nyingi zaidi na muda mrefu huku watu wakiendelea kuumizwa na magari kupata ajali. Hivyo ni vema hatua zingine zikachukuliwe ili kumaliza au kupunguza tatizo hili na kwa mtazamo wangu mzunguko huu unahitaji kufanyiwe marekebisho makubwa ili uwe mzunguko kwelikweli.
2. Tatizo Kubwa la Msongamano wa Magari hasa wakati wa Jioni na siku za Mwisho wa Wiki
1. Pamoja na uzuri na upana wa barabara hii, ni jambo la kawaidia kukuta foleni kubwa sana katika eneo hili hasa jioni na mwisho wa wiki. Karibu kila jioni utaona magari yanapambana kuchomekeana na kupita katika barabara ya akiba (service road) inayopita nje ya Kanisa la Kakobe. Nimeshuhudia ajali kadhaa wakati wa jioni kutokana na msongamano huu ambao mara nyingi unakuwa ni mrefu hadi mzunguko ulioko Mwenge
2. Kwa analysis ambayo nimeifanya kwa muda mrefu sasa, foleni hii inasabishwa na mambo kama matatu hivi:
a. Moja ni tatizo la kiufundi la mzunguko ambapo nimelieleza hapo juu
b. Mbili ni muunganiko wa barabara inayoingia Chuo Kikuu (University Road). Magari mengi sana wakati wa jioni yanaingia katika barabara hii kwa watu wanaoelekea Makongo Juu, Changanyikeni na hata wanaokwenda Kimara na Mbezi na maeneo mengine wakijaribu kukwepa foleni ya Ubungo. Titizo la kiufundi la Mzunguko huu linashindwa kukabiliana na wingi wa magari haya
c. Tatu, kutokana na wingi wa magari yanayoingia Barabara ya Chuo Kikuu, magari haya yanashidwa kupita kwa uharaka unaotakikana kwa sababu kuu mbili
i. Matumizi ya Geti la upande wa Survey la kuingia Mcimani City. Wakati huu wa jioni na mwisho wa wiki, watu wengi wanakua wanaingia na kutoka kwenye maduka na Mlimani City kwa ajili ya mahitaji binafsi. Matokeo yake, harakati za kungia na kutoka kwenye geti hili zinakumbana na wingi wa magari yanayoingia Chuo kikuu na hivyo kusababisha foleni kubwa
ii. Pamoja na uwepo wa geti hili, bado kuna kituo cha daladala nje tu ya Geti la Kuingilia Mlimani City pande zote za barabara ya Chuo Kikuu. Matokeo yake, zoezi la kushusha na kupakiza watu linaongeza ugumu wa magari kupita. Kibaya zaidi, vituo hivi viko njiani kabisa kwani hapajangwa kufanya magari yanayoshusha na kupakiza magari kutoka nje ya barabara.
Ushauri wangu katika hili
1. Moja, nashauri kuwa Lango (Gate) la kuingia Mlimani City kwa upande wa Survey liliko karibu na Kituo cha Mafuta cha Total, lifungwe na lisitumike kuingia au kutoka kwa magari. Badala yake Litumike Lango (Gate) lingine lililoko upande huohuo ambalo liko mbele kidogo karibu na kituo cha Esap. Kwa kufunga geti hili kutaongeza umbali wa geti hili kutoka mzunguko na hivyo kupunguza uwezekano wa foleni isiyo ya lazima.
2. Pili, kituo cha daladala kilichoko nje ya geti hili kifungwe na badala yake kipelekwe mbele kabla au baada ya geti ninaloshauri litumike. Kwa kuwa kituo hiki kwa sehemu kubwa kinahudumia watu wanaoingia na kutoka Mlimani City kupitia lango linalotumika sasa, kikifungwa hakitaathiri sana abiria kwani bado watakua wanashuka karibu na lango nililopendekeza kutumika.
Nina hakika Ushauri nilioutoa hapa ukifanyiwa kazi, utapunguza kabisa au kwa sehemu kubwa tatizo la ajali nyingi na msongamano wa magari usio na lazima katika eneo hili.
MM
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments