[wanabidii] KUHUSU MPANGO WA TAIFA WA KUJIANDAA NA KUKABILIANA NA MAAFA NA MKAKATI WA TAIFA WA MAWASILIANO WAKATI WA MAAFA

Monday, September 02, 2013
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA MPANGO WA TAIFA WA KUJIANDAA NA KUKABILIANA NA MAAFA NA MKAKATI WA TAIFA WA MAWASILIANO WAKATI WA MAAFA

1.  Utangulizi
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

Ndugu wana habari karibuni sana katika mkutano huu ambapo leo Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa inazungumza nanyi kuhusu Mpango wa Taifa wa kujiandaa na  Kukabiliana na Maafa na Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wakati wa Maafa.
Kama mnavyofahamu nchi yetu imekuwa ikikumbwa na majanga mbalimbali ambayo husababisha maafa.
 Maafa hayo, yapo yanayotokana na Nguvu za Asili kama ukame, mafuriko, vimbunga, magonjwa ya mlipuko nk. Vilevile, kuna maafa yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu. Mifano ya maafa hayo ni ajali za vyombo vya usafiri, Moto wa viwandani, maofisini na majumbani nk.
Ningependa ifahamike kuwa Maafa ni matokeo ya janga ambalo  huathiri kwa kiwango kikubwa mfumo wa kawaida wa maisha ya jamii kwa kusababisha vifo, majeraha, upotevu au uharibifu mkubwa wa mali au mazingira  ambayo jamii iliyoathirika isipokuwa imejiandaa na maafa haiwezi kuyakabili maafa kwa uwezo au rasilimali zake bila msaada kutoka nje ya jamii hiyo.
Kwa kuzingatia hayo  Serikali kupitia Idara yake ya Uratibu wa Maafa imeandaa Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa  unaoainisha  majukumu ya Wadau mbalimbali, kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika jamii nzima kwa kuwa na uelewa mkubwa wa kujiandaa , kukabili na kupunguza athari za maaf nchini.

Mpango huu pamoja na Mkakati wa Mawasiliano ilizinduliwa mwezi Novemba, 2012 na Waziri mwenye dhamana ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Wiliama V Lukuvi (MB) kwa wadau na kueleza jinsi itakavyosaidia kutoa muongozo wa namna ya utekelezaji wa kuratibu 
maafa katika ngazi ya Taifa.

Kama mnavyofahamu, maafa ni suala mtambuka linalomhusu kila mmoja wetu katika kukabiliana nalo, ambapo hata ninyi ndugu zangu wanahabari ni moja ya nguzo kuu ya kushiriki katika kukabiliana nayo.
 Katika Mpango huu pamoja na Mkakati wa Mawasiliano vyote vimeainisha majukumu ya kila mdau  ili kutambua ni upi wajibu wa mdau husika pindi dharura ya  maafa inapotokea.

 Tukizingatia ushiriki huo na mfumo wetu wa kukabiliana na maafa ambao una Kamati za Maafa kwenye ngazi ya mkoa, wilaya hadi kijiji ambazo zina majukumu ya kusimamia masuala ya maafa katika maeneo yao. Hivyo kila mdau ataweza kushiriki kikamilifu katika hatua zote za kujiandaa, kukabiliana na kupunguza Athari za maafa.

1.  Lengo
Kama nilivyoeleza awali, faida ya kuwa na Mpango huu pamoja na Mkakati wa Mawasiliano ni kurahisisha uratibu wa shughuli za maafa  kwa kuainisha majukumu na kuwezesha upatikanaji wa mahitaji ya msingi wakati wa dharura na namna wadau mbalimbali watakavyo shiriki katika shughuli za uratibu wa maafa na hatimaye kuweza kurudisha hali ya kawaida.
Mpango huu pamoja na Mkakati wa Mawasiliano vimeletwa kwenu Wanahabari ili ninyi wenyewe muweze kuufahamu pamoja na kusaidia Wadau wengine na wananchi kwa ujumla kutambua majukumu yao ili kila mmoja aweze kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi ili tuweze kuzuia au kupunguza athari za maafa.
Aidha serikali kwa kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa iliona umuhimu wa kuandaa Mkakati wa Mawasilianao ukiwa na lengo la kuhakikisha Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa unatekelezeka kikamilifu. Mkakati huu utakuwa ndio Dira ya kupata taarifa, kutoa elimu na tahadhari kwa Umma juu ya masuala yote yanayohusu maafa na jinsi ya kujiandaa, kukabiliana nayo pindi yanapo kuwa yametokea.
Lengo la Mpango na Mkakati huu ni kuweza kujipanga na kuwa imara katika utekelezaji mzuri wa masuala menejimenti ya maafa na dharura zinazotokana na  majanga pindi  yanapokuwa yameikumba nchi yetu.
Idara ya Uratibu wa Maafa imeona ni vyema kuja kuwaeleza wanahabari mipango iliyonayo, hii ikiwa ni katika kuboresha mawasiliano ya Maafa pamoja na namna ya kukabiliana na maafa na kupunguza ucheleweshwaji wa taarifa kutoka   katika maeneo yalipo tokea maafa nchini.
Aidha, napenda kuchukua nafasi hii kuwa taarifu kuwa Tarehe 13 Oktoba, 2013 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji Athari za Maafa Duniani. Mwaka huu (tarehe 13 Oktoba, 2013) Ofisi ya Waziri Mkuu itaadhimisha siku hiyo ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Upunguzaji wa Athari za Maafa (United Nationas International Strategy for Disaster Risk Reduction (UNISDR) limetoa kaulimbiu isemayo ''Ulemavu na Maafa, SUALA LISILOZUNGUMZWA BAYANA – Tujumuike Pamoja"
"Disability and Disasters A NOT SO OBVIOUS CONVERSATION - Join in".
Siku hii inaadhimishwa maalumu kila mwaka kwa kuwa na kaulimbiu yenye kutoa kipaumbele katika suala linalohitaji kupewa mkazo katika jamii. Kwa mwaka huu maadhimisho haya yameelekezwa katika kundi la watu wasiojiweza, yaani Walemavu ikiwa na lengo la kuwakumbusha Wadau wote wa  Maafa pamoja na jamii kwa ujumla kuwa kila mmoja ulimwenguni anahitaji Kinga dhidi ya Maafa,vilevile masuala ya Uwekezaji, Maamuzi na maandalizi ya Sera na mikakati ya Kupunguza Athari za Maafa yahusishe mahitaji ya makundi maalumu, ikiwemo walemavu.

Nawashukuru na asanteni sana kwa kunisikiliza
Imetolewa na KAIMU MSEMAJI/ OFISI YA WAZIRI MKUU

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments