Wadau.
Binafsi sijapenda wabunge wa upinzani walivyosusia kikao cha leo, ingawa inaweza kuwa na maana pana kwao.
LAKINI sijapenda zaidi wabunge wa CCM waliobaki ambao badala ya kuijadili hoja ya msingi iliyopo mezani, wametumia muda mwingi 'kupiga blaa blaa' zisizokuwa na mashiko (kwa mtazamo wangu).
Ninashindwa 'kupata picha' ya wapi wanafanya jambo lililo jema, wapinzani waliotoka nje ama wale wa CCM wanaopiga siasa na kujisimika katikati ya itikadi za kisiasa, wakiiacha hoja ya msingi pembeni?
Pongezi zangu kwa `mdogo wangu' Esther Bulaya. Nimependa sana mchango wake.
Wengine sijui mnaliona vipi hilo.
0 Comments