[Mabadiliko] Kipi Kinaanza? Kuwa na Sera, Sheria na Kanuni Kisha Mikataba ya Vitalu vya Gesi ama Kinyume Chake?

Thursday, September 26, 2013
Kuna kitu wanaita 'local content initiatives', hii kwa lugha rahisi ni mikakati ya kuwafaidisha nchi wamiliki wa raslimali za gesi, mafuta na madini. Mikakati inayotumika ni pamoja na kuhakikisha tunakuwa na kodi na mrabaha mzuri na pia mikakati mizuri inayotoa mgao stahiki kwa serikali za mitaa/vijiji kunakotoka mali hizo. Majuzi hapa nilikuwa nchini Indonesia nikajifunza kuhusu namna wanavyogawana mafao yatokanayo na uchimbaji: wao wanagawana kwenye kitalu kimoja cha gesi kampuni ya serikali yao asilimia 45, kampuni ya kigeni/wawekezaji asilimia 45 na asilimia 10 inayobakia inaenda kwenye halmashauri ya wilaya ya Bojonegoro ambako kitalu hicho kipo. Sisi Tanzania hatuna sera wala sheria ya gesi na mafuta inayoingiza haya mambo ya kisasa lakini nakumbuka kumsikia Waziri wetu wa Nishati na Madini akisema wanagawa vitalu vyao vya gesi. Hili lilinibakisha na maswali zaidi ya majibu ama furaha ambayo ingetarajiwa itokane na uwepo wa gesi na uvumbuzi wa vitalu zaidi siku hadi siku. Hivi sisi tutapata kiasi gani? Na ni lini tutakipata? mfano kule Kazakhstan wao wamesema kampuni ya wawekezaji itachimba mpaka mwisho wa ile miaka mi5 ya mwanzo kisha itatoa 'divestiture' kwa serikali ama kwa kampuni binafsi za wazawa kununua hisa zaidi ili kuwafaidisha wenyewe zaidi ya muwekezaji. Kesho nimeamua kwenda kuhudhuria breastfast meeting ya policyforum inayohusu mambo ya gesi.

--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments