[Mabadiliko] Fwd: [Engineers] MAADHIMISHO YA WIKI YA WAHANDISI YA KILA MWAKA KUHAMASISHA KUJENGA UWEZO WA RASILIMALI WATU WA TAIFA

Thursday, September 19, 2013


---------- Forwarded message ----------
From: <info@iet.co.tz>
Date: 2013/9/19
Subject: [Engineers] MAADHIMISHO YA WIKI YA WAHANDISI YA KILA MWAKA KUHAMASISHA KUJENGA UWEZO WA RASILIMALI WATU WA TAIFA
To: engineers@iet.co.tz


MAADHIMISHO YA WIKI YA WAHANDISI YA KILA MWAKA KUHAMASISHA KUJENGA UWEZO
WA RASILIMALI WATU WA TAIFA

1.      Kila mwaka tangu 2012, TAASISI YA WAHANDISI TANZANIA inatayarisha na
kuratibu maadhimisho ya Wiki ya Wahandisi. Maadhimisho haya hufanyika kote
nchini kwa wahandisi pamoja na mafundi kufanya kazi za kujitolea
wakishirikiana na wanachi.

2.      Lengo la maadhimisho haya lina sura mbili muhimu.
Kuukumbusha umma na watanzania umuhimu wa uhandisi katika maendelo ya
Taifa letu. Hakuna nchi yoyote inayoweza kupata mandeleo bila kuwepo kwa
wahandisi.

Kuwaomba na kuwahamasisha watanzania kutumia kila aina ya mbinu kujenga na
kuendeleza uwezo wa wahandisi watanzania (Local engineers).


3.      Maadhimisho haya huzinduliwa kwa Matembezi ya Hisani (Charity Walk)
yenye madhumuni ya kukusanya fedha zitakazotumika kutekeleza mradi kabambe
wa kujenga uwezo wa wahandisi wetu unaendelea kutekelezwa na Taasisi ya
Wahandisi. Ingawa mradi huu unatakelezwa kwa awamu ya miaka minne minne,
unatakiwa kuwa endelevu. Tunategemea kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka
2014, wahandisi wote wahitimu (fresh graduates) watakuwa wanaingia moja
kwa moja kazini kupata mafunzo ya kazi (internship). Hivi sasa wahandisi
wahitimu wanaachwa bila kazi wakati mahitaji ya wahandisi nchini ni
makubwa, kupita kiasi.


4.      Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika kama ifuatavyo ;
Jumapili tarehe 22/09/2013 kutakuwa na Matembezi ya Hisani (Charity Walk)
ya wahandisi wote pamoja na familia na marafiki zao. Mgeni Rasmi katika
matembezi hayo hapa Dar es Salaam anategemewa kuwa Waziri wa Ujenzi, Mhe.
Dkt. John P. Magufuli (Mb) Matembezi yataanzia ofisi za Taasisi na kuishia
kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni. Wahandisi wa huko mikoani
wamepanga ratiba zao.


Jumatatu hadi Ijumaa wahandisi kote nchini watajishughulisha na kazi
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea shule mbalimbali kuhamasisha na
kufundisha masomo ya sayansi.


Siku ya Ijumaa maadhimisho yatahitimishwa kwa kushiriki kwenye Chakukula
cha Usiku cha kila mwaka (Annual Dinner). Mgeni rasmi kwenye chakula hicho
hapa Dar es Salaam atakuwa Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu
(uwekezaji na uwezeshaji) Mhe. Dkt. Mary Nagu (MB). Tukio hili litafanyika
kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


5.      Taasisi ya Wahandisi Tanzania inaomba kama ifuatavyo ;
Watanzania na hasa wahandisi na mafundi wajitokeze kwa wingi kushiriki
kwenye maadhimisho haya. Inafaa kukumbuka kwamba matatizo na misuguano
inayoisumbua nchi yetu sasa inatokana na kuongezeka kwa ugumu wa maisha
ikiwa ni pamoja na ; ukosefu wa ajira, uhaba wa chakula, maji, nishati,
miundombinu na mengine mengi. Matatizo haya hayawezi kumalizwa kwa
mikutano ya hadhara na kulalamika. Lazima tufanye kazi na hasa kwa
kuwatumia wahandisi wetu wa ndani. Utegemezi kwa wahisani hautatusaidia.
Tuwaite wahisani kuongoza nguvu siyo kuongoza mapambano.

Waandishi wa habari wachukue hatua za makusudi kuandika mambo
yanayofanyika kutatua matatizo ya nchi baada ya kujikita zaidi kuandika
matatizo na matukio yanayotokana na matatizo hayo. Kuendelea kufanya hivyo
ni kuzidisha hamasa za uhalifu na kuwakatisha tamaa watanzania wenye nia
ya kuendeleza taifa hili.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika

Imetolewa na:
Taasisi ya Wahandisi Tanzania
Eng. Dkt. Malima M.P. Bundara
RAIS WA TAASISI
19 Septemba, 2013



Executive Secretary,
The Institution of Engineers Tanzania,
Pamba Road, Opp. Former Hotel Agig
P.O. Box 2938,Dar es Salaam, Tanzania,
Tel: +255 22 2124265/2122836,
Fax: +255 22 2124265/2115373,
Mob: +255 717 110411/0784 909060,
Emails: snakassera@yahoo.com/info@iet.co.tz
_______________________________________________
Engineers mailing list
Engineers@iet.co.tz
http://iet.co.tz/mailman/listinfo/engineers_iet.co.tz


--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments