[wanabidii] UFAFANUZI KUHUSU WAFADHILI KUJITOA KUFADHILI SHUGHULI ZA UKIMWI TANZANIA

Wednesday, August 28, 2013
TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU WAFADHILI KUJITOA KUFADHILI SHUGHULI ZA UKIMWI TANZANIA

Tume ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) – Tanzania imepata taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari kwamba wahisani wa shughuli za UKIMWI kujitoa kufadhili shughuli za UKIMWI kuanzia mwaka kesho 2014.

TACAIDS, inafafanua kwamba tetesi hizo sio za kweli hata hivyo baadhi ya Wahisani ambao wanajitoa kwenye ufadhili kutokana na miradi wanayoifadhili kuisha muda wake au kubadilika vipaumbele kwa mfano Serikali ya Kanada na Denmark ambao wamekuwa wakisaidia Programu za UKIMWI kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na Jamii ambapo mradi wao unaisha 2016/17. Hata hivyo Serikali ya Denmark bado ina nia ya kuendelea kusaidia shughuli za UKIMWI, baada ya Mradi huo kuisha.

Utekelezaji wa shughuli za UKIMWI Tanzania umekuwa ukipata ufadhili wa fedha kutoka Serikali ya Tanzania na Serikali za Nchi Marafiki. Programu zinazotekelezwa hufuata Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NMSF).Mpaka sasa kuna uhakika wa fedha za UKIMWI kwa miaka mitano (5) ijayo.

Serikali za nchi Marafiki wamekuwa wakisaidia shughuli za UKIMWI kwa mtindo wa Miradi (Projects) ambayo ni
ni ya muda mfupi kama vile miaka mitatu (3) mpaka mitano (5). Kwa kawaida miradi huisha na mingine huanza kila mwaka. Kwa sasa hivi miradi mingi inatekelezwa kwa kipindi cha Maisha ya Mkakati wa nchi wa UKIMWI ambao unaisha mwaka wa fedha 2017/18. Wahisani wakubwa wa shughuli za UKIMWI ni Serikali ya Marekani na Mfuko wa Dunia wa Magonjwa ya UKIMWI, Kifua kikuu na Malaria. Wahisani hawa wawili wanatoa kiasi cha 80% ya fedha za UKIMWI nchini na ndio wanaofadhili Programu ya Tiba ya UKIMWI nchini na Programu zao bado zinaendelea na hawajatangaza kujitoa.

Baada ya Miaka 30 ya shughuli za UKIMWI, Tanzania sasa hivi inafahamu maambukizi ya VVU makubwa yanapatikana katika maeneo gani ya Jamii. Mfano; Makundi ya Wanandoa, Wauza ngono, Wanaofanya ngono ya jinsia moja, Wanaotumia dawa za kulevya na Maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto. Hivyo mikakati mingi sasa hivi inaelekezwa katika maeneo hayo ikiwamo kuongeza Tiba kwa WAVIU ambao wanapata tiba vizuri inakuwa ni kinga kubwa hata kwa wenzi wao.

Serikali ya Tanzania baada ya kupata uzoefu wa miaka yote hii inaelekeza nguvu kwenye maeneo ambayo yataleta matokeo makubwa na mazuri zaidi ili kufanikisha haya, Serikali iko katika hatua za mwisho za kuanzisha Mfuko wa UKIMWI Tanzania (AIDS TRUST FUND). Mfuko ambao utachangiwa na Serikali, Wadau wengine nchini pamoja na Wadau wa Maendeleo. Mfuko huu unakadiriwa kupunguza utegemezi wa Wahisani kwa 50%.

Mfuko huu unategemewa kuanza Mwaka wa Fedha 2014/2015.

Imetolewa na: Mwenyekiti Mtendaji
Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS)
Sokoine Drive/Luthuli Street,
P. O. Box 76987
Dar es Salaam.
Tel: +255 22 2122651/2122427,
Fax: +255 22 2125651,
Email: ec@tacaids.go.tz 
Website: www.tacaids.go.tz

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments