[wanabidii] Rais wa SMZ Dk Shein afanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

Tuesday, August 20, 2013

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
      Zanzibar                                                                                     20.8.2012

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 amefanya marekebisho katika muundo na majukumu ya baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kufuatia marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika Wizara nyengine. Marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo zinaendelea kubaki Wizara 16.

Shughuli za Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ zimeondolewa katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kuundiwa Wizara mpya.

Shughuli za Utawala Bora zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora na 
kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Shughuli za kazi zimeunganishwa na shughuli za utumishi na kuundiwa Wizara mpya.

Shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika zimeondolewa kutoka Wizara ya Kazi,  Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi na Ushirika na kuunganishwa na shughuli za ustawi wa jamii, vijana, wanawake na watoto.

Shughuli za Tume ya Mipango zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Aidha, kufuatia kuundwa kwa Wizara hizo mpya Rais Dk. Shein amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Wizara kwa kuwabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora anakuwa Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame na katibu Mkuu wake anakuwa ndugu Salum Maulid Salum ambapo Naibu Katibu Mkuu ofisi hiyo anakuwa Said Abdulla Natepe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, anakuwa Mhe. Haji Omar Kheir na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo anakuwa ndugu Joseph Meza ambapo Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa ni ndugu Mwinyiussi A. Hassan na Naibu Katibu Idara Maalum za SMZ anakuwa CDR Julius Nalimy Maziku.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma anakuwa Mhe. Haroun Asli Suleiman na Katibu Mkuu wake anakuwa ndugu Fatma Gharib Bilal na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma anakuwa ndugu Yakout Hasan Yakout.

Wizara ya Fedha itakuwa chini ya Waziri Mhe. Omar Yussuf Mzee na Katibu Mkuu wake ni ndugu Mussa Omar na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo atakuwa ndugu Juma Ameir Hafidh.

Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto anakuwa Mhe. Zainab Omar Mohamed ambapo Katibu Mkuu wake atakuwa ndugu Asha Ali Abdalla na Naibu Katibu Mkuu Uwezeshaji na Ushirika atakuwa ndugu Ali Khamis Juma na Naibu Katibu Mkuu Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto atakuwa ndugu Msham Abdalla Khamis.

Wakati huo huo, Dk. Shein anatarajia kuwaapisha viongozi hao jioni hii ya leo.

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822  
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments