[wanabidii] CUF YALAANI KUMWAGIWA TINDI KALI KWA WAGENI Z’BAR

Saturday, August 10, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 7/08/2013

Kila mwananchi wa Zanzibar ameshitushwa na kusikitishwa na tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Kiengereza usiku tareh 7 Agost 2013 huko katika maeneo ya Mji mkongwe Zanzibar yaliopo mahoteli mengi na makazi ya wageni wanaotembele nchi yetu kutoka sehemu mbali mbali duniani.

Chama Cha wananchi CUF kinalaani kwa nguvu zote tukio hilo la kikatili la kuwamwagia tindi kwa wageni wetu hao,na kinalitaka Jeshi la Polisi Zanzibar kufanya uchunguzi wakina na waharaka pamoja na kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na tukio hilo la kikatili  wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Matokeo haya ya kikatili ya kumwagiwa kwa watu tindi kali yamekuwa yakishamiri siku hadi siku ndani ya visiwa vya Zanzibar,ambayo yamekuwa  yamewathiri watu kadhaa tena bila ya wahusika kuweza kupatikana na kuchukuliwa hatuwa za kisheria kiasi ambacho sasa jamii ya wazanzibar imejengeka katika hofu juu ya  usalama wa maisha yao ya kila siku,Hii ni dalili mbaya kwa Nchi ya Zanzibar kwani matukio haya ya tindikali yamekuwa yanaonekana kama ni masuala ya kawaida jambo ambalo linatishia uchumi wa Visiwa vyetu.

Kufanyiwa hujuma raia hao wakike wawili wa kigeni kutoka nchini Uengereza kigeni ambao walikuwa Zanzibar kwa kazi za kujitolea (valantia) kusomesha katika skuli za msingi (primary)
ni dhahiri kuwa  Sekta muhimu inayotegemewa katika kukuza uchumi wa Zanzibar (utalii)inaweza kutetereka.

Chama cha wananchi CUF kinawataka wananchi wote wa Zanzibar kutoa kila aina ya mashirikiano ya kuweza kufanikisha kukamatwa wahalifu hao na hatimae kufikishwa katika sehemu husika.

Sambamba na hilo Chama cha wananchi CUF Kinawataka Wanachi wote, Polisi jamii kutoa kila aina ya mashirikiano kwa Jeshi la Polisi ili jeshi hilo liweze kukomesha kabisa vitendo vyote vya kihalifu ndani ya nchi yetu, kwa lengo la  kuiendeleza sifa ya asili ya zanzibar isemayo kuwa Zanzibar ni njema atakae na aje…

Haki sawa kwa wote.

Salim A Biman

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments