Ndugu zangu,
Leo nikiwa nimesimama pale Ubungo Mataa niliingiwa na huruma kwa trafiki wa usalama barabarani aliyekuwa akiyaongoza magari. Kazi yake ni ya hatari, achilia mbali hatari ya kugongwa na madereva wazembe, lakini kubwa lingine ni afya yake.
Nimefikiri juu ya moshi wa magari na vumbi la barabarani ilihali trafiki yule hana hata cha kumkinga na vyote hivyo puani na mdomoni.
Hivi, Kamanda wa Usalama Barabarani anashindwa kuwasaidia trafiki wake hata kwa hayo ya msingi tu.
Na hakika, trafiki mara nyingi ni watu wenye kulaumiwa sana, lakini, kila inapotokea ajali, mara nyingi wao ndio huwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kutoa msaada. Na bado mazingira ya kazi zao ni magumu sana.
Tunajua pia, kuna trafiki wenye kujihusisha na vitendo vya rushwa, lakini, siamini kuwa trafiki wote ni wala rushwa. Kufikiri hivyo ni kuwaonea.
Maggid,
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments