Imeandikwa na Mwandishi Maalum — Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Edward Lowassa (Mb) amesisitiza haja na umuhimu wa kuwapo kwa ubia kati ya serikali na sekta binafsi katika kuzikabili changamoto zinazotokana na ongezeko kubwa la idadi ya wazee.
"Maisha Zaidi ya miaka 60 hayapaswi kuwa ya utegemezi, unyonge, kutojiweza au kutokuwa na matumaini. Wazee bado na wanao mchango mkubwa ndani ya jumuiya, jamii, na familia zao ili mradi tu wawezeshwe".
Na kwa sababu hiyo anasema Mhe. Lowassa, juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea Tanzania ikiwamo za utoaji wa huduma za msingi kama vile Afya, pensheni na uwezeshwaji, zinapaswa kuchagizwa na sekta binafsi.
Mhe. Lowassa ameyasema hayo siku ya Jumatano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wakati

aliposhiriki majadiliano kuhusu namna gani suala la Wazee linavyoweza kuingizwa katika ajenda za maendeleo baada ya mwaka 2015.
Majadiliano hayo yaliandaliwa na United Nations Foundation kwa ubia na International Federation of Ageing, Help Age International, AARP, Global Coalition on Aging, mHealth Alliance na Pfizer.
"Kama kundi hili la wazee likiwezeshwa na kusaidiwa ipasavyo, linaweza kuipatia jamii soko jipya, ujasiriamali, utoaji wa maamuzi, utoaji wa huduma na utalaamu anuai katika maeneo ya sayansi, teknolojia na upatanishi" anasema Lowassa
Na kuongeza, ili hayo yote na mengine mengi yaweze kufanikiwa panahitajika bajeti ya kutosha kwa ajili ya kundi hilo la jamii ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya pensheni, huduma za afya ambazo zitakidhi mahitaji ya wazee, huduma za kisaikolojia na huduma za ulinzi jamii.
Hata hivyo anasema, inasikitisha kwamba, katika nchi nyingi za Afrika na nyinginezo hata zile zilizoendelea bado haziwezi kutoa huduma za uhakika na zenye viwango vya kukidhi mahitajio ya wazee.

"Mara nyingi huduma kwaajili ya wazee inabidi zishindane na huduma za makundi mengine kama vile ongezeko la vijana wasiokuwa na ajira, upunguzaji wa vifo vya watoto wachanga na wanawake wajawazito. Hata hivyo pamoja na changamoto zote hizi za vipaumbele hatuwezi kuendelea na utaratibu huu wa kuchagua. Lazima tutumie maandalizi ya ajenda za maendeleo baada ya 2015 kuwahudumia wazee" anasisitiza Lowassa.
Akasema Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kujikumbusha na kujifunza kwa kosa la kutoingiza suala la Wazee katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) yanayoelekea ukingoni, kwa kuhakikisha kwamba Wazee wanaingizwa katika malengo mapya ya maendeleo baada ya 2015 kwa kuwa ni suala ambalo haliepukiki
Akizungumzia hatua mbalimbali zinazochuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwahudumia wazee, Mhe. Lowassa anasema kama ilivyo kwa nchi nyingine, Tanzania nayo inakabiliwa na ongezeko la idadi ya wazee.
Kwa mfano, amesema asilimia 4.5 ya idadi ya watu, ni watu walio na umri wa miaka 65 wastani wa juu zaidi kuliko ule wa asilimia 3.6 Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
"Asilimia 80 ya watu hawa wanaishi vijijini na maisha yao yanategemea kilimo. Serikali inajitahidi kadri iwezavyo kutoa huduma za msingi kwa kundi hilo ingawa pia, na kama ilivyo kwa nchi nyingine, tunakabiliwa na changamoto nyingi kukidhi mahitaji yote ya wazee," alibainisha.
Akatumia pia fursa hiyo kuyashukuru mashirika ya kimataifa kama vile Help Age International ambalo limekuwa likiendesha shughuli zake nchi nchi tangu mwaka 1993.
Akatoa mfano kwa kusema Shirika hilo, mwezi Juni mwaka huu kwa kushirikia na Pfizer limezindua mpango wa miaka miwili wa kupunguza athari zitokanazo na magonjwa yasiyoambukiza (NCD) ambayo yamekuwa yakiwaathiri wazee.
Akasema utoaji wa huduma hiyo unakwenda sambamba na juhudi za serikali katika kukabiliana na magonjwa hayo.
Akatoa wito kwa mashirika mengine kuiga mfano huo na kwamba serikali itakuwa tayari kushirikiano nayo,
Takwimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu ( UNFPA) zinaonyesha kwamba, katika kila sekunde watu wawili duniani wanaadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa kwao, na kwa mwaka karibu watu milioni 58 wanaadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa.
Aidha katika kila watu nane, mmoja ana miaka 60 au zaidi na makadirio yanaonyesha kwamba ifikapo mwaka 2050 katika kila watu watano mmoja atakuwa na miaka 60 au zaidi.
Ongezeko la idadi ya wazee duniani linachangiwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na ongezeko la umri wa kuishi ambapo katika nchi 33 raia wao wanaishi zaidi ya miaka 80 wakati miaka mitano iliyopita nchi ambazo umri wa kuishi ulifika miaka 80 zilikuwa 19 tu.
Utafiti zaidi unaonyesha, umri wa kuishi utaongezea hadi kufikia miaka 90 au hata miaka 100. Japani kwa sasa ndiyo inasemekana kuongoza kwa kuwa na asilimia 30 ya wazee lakini ifikipo mwaka 2050 nchi 64 zitaungana na Japani kwa kuwa na asilimia 30 au zaidi ya wazee.
Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/07/lowassa-awasemea-wazee.html#ixzz2YiKIs4ub
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments