[wanabidii] Kutokubalika kwa muungano wenye serikali mbili na tatu

Friday, July 26, 2013
Nionavyo mimi suala la uraisi kwa zamu linawezekana. Kwa vipi? Kikatiba vyama vya siasa vipewe uwezo wa kumteuwa mgombea wao wa uraisi ambaye atakuwa na uwezo wa kumteuwa makamu wake kama ilivyo marekani-US. Iwapo mgombea urais atatoka Bara, basi makamu wake amchague kutoka Zanzibar na iwapo ni zamu ya mgombea kutoka Zbar, basi makamu wake atoke Bara. Ili kufanikisha suala hili iwe kisheria kuwa vyama vyote viwe na wafuasi nchi nzima, yaani Bara na Visiwani. Wananchi watakuwa na fursa kumchagua kiongozi wanaemuona anafaa bila kujali ni w na chama kitatawali kwa maadili kilichapanga. Ni baada ya kipindi cha utawala kupita wananchi wataona manufaa au machafuzi ya chama tawala.

Kuhusu kuwepo na serikali tatu sio jambo zuri kwani litazidi kuongeza utengano. Serikali ya ndani ya Zanzibar wacha tu iendelee, ila inapaswa kuelewa mamlaka yake na ya muungano. Kinyume ni hivyo mvutano utakuwapo siku zote. Pande zote mbili lazima zielewe na kufuata masharti ya muungano. Tanzania Bara, yaani Tanganyika sio lazima tuwe na serikali yetu, wingi wetu unatosha kujisikia kuwa nchi ni yetu. Uchache wa ndugu zetu wa Wisiwani unawafanya kutojiamini katika umilikaji wa maslahi yetu sote kama nchi. Ndio maana wanakuwa walalamikaji kwa kila kitu. SORRY FOR SAYING THIS, bali hiyo ndio hali halisi.
Mtanganyika

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments