[Mabadiliko] KUIBIWA RESEARCH DOCUMENTS NA LAPTOP

Friday, July 12, 2013
Ndugu zangu,

\Jana usiku wakati natoka kwa mdogo wangu, nikiwa maeneo ya Mlimani City, gari langu lilikzima ghafla. Nilikuwa nimelitoa kwa fundi jioni.

Baada ya kuhangaika hapo, akaja kijana dreva taxi akajifanya ananisaidia. Akapendekeza tutoke kwenye mzunguko (roundabout) tusogee pembeni karibu na kituo cha mafuta "bonjour". Tulipofika akasema niwashe gari, baadae akaniambia betri ziko na nguvu kidogo, na yeye ana betri ndogo, hivyo gari haliwezi kuwaka. Akashauri tulisukume mpaka Mlimani City tuwakabidhi walinzi wa pale.

Nikapendekeza tuiwache hapo "bonjour" sehemu ya Subway restaurant. Yeye akasema anaenda kuita vijana wa kutusaidia, na mimi nikasema ngoja niwataarifu walinzi. Lilikuwa kosa. Yule kijana, ambaye namba ya gari wala namba ya ubavuni sikuikariri, akafungua gari(hakwenda kwa wale vijana) akakwapua begi na kuondoka kwa mwendo kasi.

Ndani ya begi kulikuwa na kompyuta mpakato(laptop), reseasrch materials zangu zote, flash disks nilimokuwa nimeweka Chapters 3 (tatu) za thesis yangu na vitu vingine vidogo.

Nimeathirika na sina hakika kama sikupata angalau hizo materials na flash, kama nitaweza kuendelea na masomo.

Nawaomba mniombee ili niweze kuambulia chochote kati ya hivyo, vinginevyo nguvu na jitihada zangu zinaweza kuwa zimekomea hapo.

Iwapo mtu atapata taarifa zozote, labda za kuokotwa begi na mavitabu anaweza kuwasiliana nami kwa
namba hizi:

0788 275 801
0754 284 508


Natanguliza shukrani.

Ndugu yenu, Lugaziya, M.J

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments