Ndugu zangu,
Jioni hii baada ya mazoezi ya mpira wa watoto niliongozana na makamanda wangu hadi mitaa ya kati ya Iringa. Nilifika maeneo ya Stendi Kuu, Mashine Tatu na hata Soko Kuu. Hali ya utulivu imerejea. Sikuona hata polisi mmoja barabarani.
Baadhi ya shughuli za biashara zimerejea kama kawaida. Lakini, la msingi, katika miaka yangu kumi ya kuishi hapa Iringa hili ni tukio la kwanza la aina yake.
Bado naamini, kuwa hili la Wamachinga na Manispaa ni jambo dogo ambalo, kama wahusika watatanguliza hekima na busara, linaweza kumalizwa mezani na kunusuru amani na utulivu wa Mji wa Iringa.
Maana, katika nchi za wenzetu kwa yaliyotokea leo wangefanya pia mahesabu ya hasara ya kiuchumi iliyotokana na kusimama kwa shughuli za kiuchumi.
Maana, kama mtu atapiga hesabu za haraka tu kuangalia machache yafuatayo: Gharama za mafuta na posho kwa idadi ya magari ya polisi yaliyotumika, idadi ya polisi walioshiriki zoezi la leo. Idadi ya mabomu yaliyotumika leo na gharama yake.
Iangaliwepia hasara ya kimapato kwa idadi ya maduka yaliyofungwa kwa siku ya leo. Daladala zilizoshindwa kufanya kazi. Achilia mbali mali zilizoharibiwa.
Maana, kadhia kama hii ya leo imepelekea kupungua kwa kiasi kikubwa cha mzunguko wa fedha na hivyo kuwaathiri wengi kiuchumi.
Ni dhahiri, kuwa ni muhimu kwa Wamachinga wakatafutiwa namna ya kufanya kazi yao ya kujipatia riziki, lakini, itangulizwe pia hekima na busara katika kulitafuta jawabu ili kuepusha madhara ya kiuchumi na kijamii.
Ni matumaini yetu, kwa mji wetu wa Iringa na Mkoa wetu kwa ujumla, tukio la leo liwe pia fundisho la kubaini njia bora za kutatua migogoro yetu , ya kisiasa na kijamii. Na hakuna njia iliyo bora kabisa, kama njia ya mazungumzo.
Na kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine ya kutufikisha hapa, basi, watafakari kwa makini, ili kilichotokea leo kisitokee tena, kama inawezekana.
Maggid,
Iringa.
0754 678 252
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en ---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/groups/opt_out.
Share this :
0 Comments