[wanabidii] Tukumbushane Neno; Falsafa Ya Mtungi..

Sunday, March 10, 2013


Ndugu zangu,
Asubuhi moja nikiwa kwenye mchakamchaka ( jogging) nilimsikia mchungaji wa kanisa akiwatamkia waumini wake;

" Angalieni upepo, nguvu ya upepo. Duniani upepo unaweza kutingisha miti, ukavunja matawi na hata ukaangusha miti….!" Sikusimama nikasikiliza alichotaka kusema Mchungaji yule juu ya upepo na nguvu zake. Lakini, nami nikaanza kutafakari na kujiuliza; Matatizo yetu wanadamu na hasa sisi Watanzania ni nini?

Nikafikiri, kuwa mara nyingi Watanzania hatutaki kuyajua matatizo yetu. Tunataka kuyajua ya wenzetu. Na tukiyajua yetu, hatutaki kuyaweka wazi. Tu mahodari wa kusiliba matatizo yetu. Nje hayaonekani, yamesilibiwa, lakini, ndani hali iko vile vile.

Tuliokaa vijijini tunajua, kuwa nyumba ya kijijini haijakamilika bila kuwa na mtungi. Afrika hakuna tu siri ya mtungi, kuna falsafa ya mtungi pia. Ninapoingia kwenye nyumba kijijini huangalia kwanza ulipo mtungi.

Kwenye mtungi yawezekana ndimo yalimo maji ya kunywa. Na ukiinamia mtungi wa maji, usiaangalie sana, chota maji yako, kunywa. Lakini, mtungi pia hutumika kuhifadhia vyakula; iwe unga au maharage. Mara nyingi mtungi huwekwa kwenye kona ya chumba. Na mtungi ukikaa sana, basi, siku ukiinuliwa, huacha alama.

Na unafanyaje basi mtungi wa maji unapoonyesha kuwa na nyufa, kuwa maji yameanza kuvuja? Kuna mawili; la kwanza si la busara sana. Ni jawabu la muda mfupi, la pili ni la busara zaidi, ni suluhisho la muda mrefu.

Afrika mtungi wenye nyufa unaweza kuzibwa kwa kusaga vipande vya mtungi wa zamani, kisha ukachanganya na nta. Baada ya hapo utasiliba kwenye nyufa za mtungi. Hiyo ni njia ya kwanza, ni suluhisho la muda mfupi.

Maana, tabu inakuja, siku mtungi utakapohitajika kuchemshia ' komba'- togwa la pombe. Basi, kwenye moto mkali wa kuni nyufa zile, pamoja na kusilibwa na nta, hazitahimili nguvu ya moto. Mtungi utamegeka vipande vipande. ' Komba', ama togwa la pombe litamwagika.

Naam, dawa ya mtungi wenye nyufa si kusiliba kwa nta, ni kufinyanga mtungi mpya, basi. Na jamii yetu imekuwa ni kama ya ' Super- glo', ile gundi inayoaminiwa inaweza kusiliba , ama kuunga chochote kile. Kila jambo tunakimbilia kuitafuta ' Super-glo'. Kama nta, Super-glo nayo haihimili kwa muda mrefu joto la moto, au hata la jua.

Wanadamu tuwe na ujasiri wa kuyatambua matatizo yetu kama yalivyo. Tusiwe wepesi wa kukimbilia ' kusiliba' kwa nta au super-glo. Mengine ni ya kuyafanyia mabadiliko ya jumla.

Natamani nikutane na Mchungaji yule wa Kanisa, aniambie, kuwa kwake alikuwa na maana gani aliposema kuwa upepo ni tatizo. Tafakari.

Maggid Mjengwa,

Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz/

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments