[wanabidii] Waziri Mkuu aunda Tume kuchunguza Matokeo ya Form 4

Saturday, February 23, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi
wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka
huu.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya
wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo
ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha
wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania
Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges
(TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia
masuala ya elimu.

Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya
Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari
Tanzania (TAHOSSA).

Amesema Serikali inawaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi
wote kwa ujumla watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake
kwa ufanisi.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, FEBRUARI 23, 2013.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2LjAo1K4B

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments