[wanabidii] SHAMRA SHAMRA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI @36

Sunday, February 03, 2013
Mr Yona,
Tanzania inayumba sana katika kila sector. Insikitisha sana kwamba watu ambao mna uwezo wa kuwaelimisha watu ili wapate kuelewa winavyo fanyika huko, mnakuwa ni wapiga propanganda tu. Historia ya Tanzania, kuanzia enzi za utawala wa machifu inaonyesha jinsi UMOJA ULIKUWA NI NYANZO MUHIMU KTK MAENDELELEO YA JAMII ( eg. vita ya maji maji, harakati dhidi ya ukoloni -n.k, nk) Leo hii, umoja haupo badala yake - udini, ubabe rushwa, upinzani, usalama upo mdogo ni vitu ambavyo vinaonekana usiku na mchana. Baada ya miaka 50 ya uhuru nchi haina maji, umeme, chakula cha kutosha, usafiri hafifu- reli ya kati imekufa na bado unasema nchi chini ya chama tawala haiyumbi? Hata michezo hatusikiki duniani kabisa. Sasa hayo mambo ya kusifiana yanamsaidia nani? For sure, hayamsaidi mwananchi wa kawaida. Matokeo yake ni kwamba wanaotawala wataendelea kufanya makosa wanayoyafanya hivi sasa na wapinzani wataendelea kupinga hata kana kwamba wataona ukweli na watoto wetu hakuna chochote kizuri wanachojifunza, basi nishida tu. I'mnot against anybody, but whoever comes to power or rules must think of a country as a single unit and make people know what is going on in their country. Pamoja na kwamba naishi abroad, lakini bado na kadi ya CCM ambayo niliipata JKT-OLJORO miaka 2 baada ya kuanzishwa CCM. I'm proud of it because it's part of our history. Lakini haina maana kusifia mambo mabaya yanayosababisha nchi kutoendelea. Hizo SHAMRA SHAMRA NI ZA NANI NA KWA NINI wakati hapo Dar hakuna umeme, maji, ujambazi unakolea. Ukweli lazima usemwe Mr Yona ili tujirekebishe, na sio kupiga madebe ili kuwafurahisha baadhi tu ya wananchi. Mtanzania ni Mtanzania tu, whether ni mwana CCM au MPINZANI, wote tunachitaji maendeleo ili hali zetu ziwe nzuri.

Mtanganyika

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments