Na Mwandishi wa Thehabari.com Korogwe
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Bungu iliyopo Korogwe Vijijini wamelalamikia kitendo cha baadhi ya
walimu wao kucheza mchezo wa table tennis ofisini (staff room) tendo ambalo limekuwa likifanyika hata
wakati wa kazi/vipindi vya masomo. Malalamiko hayo yametolewa juzi ambapo mwandishi wa Thehabari.com
alitembelea shule hiyo kuangalia changamoto mbalimbali za elimu eneo la Korogwe Vijijini.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao kiusalama na mwandishi wa habari hizi baadhi ya
wanafunzi hao walisema wapo walimu ambao wamekuwa wakicheza mchezo huo hata wanapokuwa na vipindi jambo
ambalo huwakatisha tamaa wanafunzi. "Wapo baadhi ya walimu wamekuwa wakijisahau na kucheza table tennis
hata kama ni muda wa vipindi...na endapo akiwaanacheza na kiongozi wa darasa asimfuate kumkumbusha
kipindi anaweza asije kabisa," alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Thehabari.com ilifika shuleni hapo na kuingia hadi ofisi ya walimu (staff room) na kushuhudia meza ya
table tennis ikiwa imefungwa katikati ya ofisi hiyo tena ikipewa nafasi kubwa zaidi ya vifaa vingine vya
kikazi vya walimu hao.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alipozungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari Bungu,Dismas Kimweli
kutaka kujua sababu ya shule hiyo kuweka uwanja wa table tennis ofisini hapo mwalimu huyo alisema
wameufunga kwa muda kutokana na kukosa eneo la kuuweka, lakini wanafanya jitihada za kuutoa uwanja huo.
"Ni kweli eneo hili kufungwa uwanja kama huo si sahihi...hili nalielewa lakini tuliufunga kwa muda tu na
hivi sasa tunajiandaa kuuamisha," alisema Kimweli. Akifafanua zaidi alisema kutofundishwa kwa baadhi ya
vipindi kwa wanafunzi hakutokani na michezo ya table tennis shuleni bali uchache wa idadi ya walimu
shuleni hapo. Alisema kutokana na uchache huo wa walimu baadhi ya mwalimu huwa na vipindi karibia 70 kwa
wiki jambo ambalo huwazidi baadhi yao hivyo kujikuta wakitupiwa lawama.
Shule ya Sekondari Bungu iliyoanzishwa mwaka 1989 yenye jumla ya wanafunzi 640 ina walimu 12 tu huku
kati ya idadi hiyo walimu watatu wako masomoni.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Maelezo ya Picha Picha mbili juu zinaonesha meza ya table tennis akiwa ndani ya ofisi ya walimu.
_________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments