[wanabidii] CCM TAMBUENI KIBAYA CHAJITANGAZA KIZURI CHAJIUZA

Tuesday, December 18, 2012

Richard Makore <rmakore@gmail.com>
5:23 PM (0 minutes ago)

to mabadilikotanz.


Ndugu zangu tuwaulize hawa CCM watatumia shilingi ngapi, na je kwa nini hizo fedha wasizitumie kuchimba visima watu wapate maji? kulipia katika TV hizo ni gharama kubwa,mfano ukitumia TV 3 gharama yake sio ya chini ya Sh. milioni 10 naamini hivyo, kuchimba kisima kimoja cha kuwasaidia watu zaidi ya 100,000 ni Sh. milioni tano ukitumia Sh. milioni 10 maana yake ni sawa na kuwanyimka haki ya kupata maji wananchi 200,000 kutoka visima viwili vikubwa,
 
Kibaya zaidi hawa jamii wanasema zoezi hilo ni endelevu, mimi sijui hiyo bajeti yake inatoka CCM ama serikalini, na kama ni serikali ilitengwa kupitia wizara gani?, mtu ukifanya kitu kikaonekana huna sababu ya kutumia tena gharama kukitangaza.
 
Kwa mfano, jimbo la mheshimiwa Nimrod Mkono mkoani Mara la Musoma vijijini, amechimba visima, amejenga barabara, amejenga shule za msingi na sekondari kwa kifupi amefanya vitu vya misngi, ukifika muda wa kampeni hapigi tena kampeni anawaambia twende pale tukafungue hiki mara twende pale tukafungue mradi huu.
 
 
Hiyo ni dhana ambayo wananchi wanahitaji na sio ujanja ujanja mara wa kutuma mawaziri mikoani, mara CCM iondoke na mawaziri ooo mara kwenye TV hapana hiyo haifai.
 
Mliahidi Meli, mwaka 2010 kwenye kampeni mkizinunua hamtakuwa na haja ya kwenda kuwatangazia watu kwa kuwa wataziona kwa macho, barabara za juu mkijenga wakazi wa Dar es Salaam wataziona, majenga ya Machinga kila Manispaa jengeni wamachinga watayaona, tatizo la maji Dar kuwa historia leteni maji muone kama wananachi watataka matangazo yenu kwenye TV ili kuwaonyesha.
 
Ndugu nina mengi ya kusema lakini ngoja niishie hapa ahadi kibao utekelezaji 0 naitwa Makore 0713608317

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments