[wanabidii]

Monday, November 05, 2012
Binafsi ninajua na kutambua kuwa uwezo wa kuwapiga Wamalawi na krejesha maji yetu tunao tena hata wa kikifanya nchi ya Malawi kuwa mkoa mkubwa wa Tanzania. lakini tutambue kuwa vita ina gharama zake na si kidogo.
 
Hapa ndipo tunapotakiwa kutambua falsafa ya Collin Powell wa Marekani katika vita kwamba tukae chini tupige mahesabu. Kama tutajiridhisha kuwa faida tutakayopata ni kubwa maradufu tukipigania ziwa Nyasa kuliko hasara tutakayopata tukisalimu amri, hapo tuanze kunoa mundu na mapanga.
 
Kwa hilo hata mimi naomba magwanda nitakuwa mstari wa mbele kutetea nchi yangu. Lakini tusishabikie vita kimzaha. Na pia tusiidharau Malawi kwa udogo wa eneo na jeshi maana hata Daudi, kijana mdogo alimtandika Goliath hadi sakafuni. 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments