Katika pita pita zangu nimekutana na hili huko Jamii Forums. Naomba watumishi na wanajukwaa hapa tusome halafu hebu watuambie je hili ni kweli kwao....??
"Ufisadi umeshakuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Haishangazi leo mtumishi wa umma akiwa mwadilifu (yaani asipokwapua fedha za Serikali) anaonekana mbumbumbu na mshamba. Leo hii ukienda kutafuta huduma yoyote Serikalini (Hata ile ya kutaka faili lako lishughulikiwe) utatakiwa kutoa fedha/rushwa ili mambo yasogee.
Taratibu, rushwa iliyokuwa ikihusisha mtanzania mmoja mmoja dhidi ya mfanyakazi mmoja wa umma sasa imebadilika. Imekuwa more complex. Rushwa imekuwa institutionalized. Hata wafanyakazi wa ofisi moja sasa wanatoa rushwa ili mafaili yao yasogee au wapandishwe vyeo.Bureaucracies zimekuwa nyingi, rushwa imekuwa damuni sasa.
Nenda maofisini, watumishi wa umma ni mabingwa wa kubuni safari, kuforge receipts za usafiri na manunuzi ili kubaka fedha za walala hoi. Vichwani mwao wameishiwa ubunifu wa kuwatumikia watanzania, wamefikia mwisho. Wakifika kazini kutwa nzima wanapanga dili za kukwapua fedha za umma. Utumishi wa umma umeoza kabisa, umebaki kwneye mifupa tu.
Commonality katika rushwa kwa mtanzania mmoja mmoja na taasisi za Serikali imetokana na usugu wa ufisadi kutoka kwa majina hayo yaliyo kwenye List of shame. Nchi inatafunwa, hakukna hatua zozote zinazochukuliwa. Ni kama kuna mashindano ya kuitafuna nchi ambayo yamekosa mwamuzi (Referee). Kila mtu anatafuna kwa uwezo wa kamba yake.
Kati ya eneo ambalo hata chama kingine kikichukua dola kitakuja kuhangaika nalo ni Mfumo mzima wa utumishi wa Umma. Unahitaji kufumuliwa na kusukwa upya. Bila shaka CDM waanze kwa kupanga mikakati ya kuboresha eneo kada hii ni kama imekufa na imeishiwa " Source: Jamii Forumn.

Wanajukwaa mnasemaje tujadiliane je ni kweli, kama ni kweli kwa kiwango gani na nini kinaweza kufanyika kwa vile hapa ndipo moyo wa maendeleo ya taifa ulipo. Siamini kama unaweza kuondoa wote na kuanza na wapya kabisa kwenye Serikali kama itawezekana.....TUJADILIANE.
K.E.M.S.
0 Comments