lile kwani kwa hali inavyokwenda Zanzibar hapana usalama wa Raia tena.
Serikali iliopo imeshindwa kwani wao binafsi ndio chanzo cha matatizo
Zanzibar.
Nasema hivi kwa mantiki ya kwamba Viongozi na Serikali ya Mapinduzi
imeshindwa kulinda usalama wa Raia wake matokeo yake wao binafsi
wamekuwa ni maadui wa Raia zao,kuwatesa na kuwatupa Magerezani bila
hoja ya msingi.
Ushahidi upo kwamba wao ndio wanaondaa mipango hii yote.Lengo ni
kuifanya Zanzibar kuwa na mtafaruku wa wenyewe kwa wenyewe ili malengo
ya Wahafidhina yatimie.Uamsho ni kisingizio tu lakini kiini cha
matatizo haya ni Viongozi wa serikali ya Zanzibar kushikwa shemere na
Tanganyika.
Rais ameshindwa kuendesha Serikali badala yake amekuwa ni mshika
usukani tu,usukani ambao unaelekezwa kila upande hata kama gari
itaingia msingini yeye hana habari, alimradi yeye amepinda kona
tu.Nchi kama Nchi haiwezi kuongozwa kwa fitina na majungu kila uchao.
Rais Shein na Viongozi wenzake wanashindwa kuelewa kwamba wanawaongoza
binaadam na sio wanyama wana fikra na maarifa yao.
Matukio yote ambayo yanatokea Zanzibar ni njama zilizopangwa na
Tanganyika na kupata baraka zote za Wahafidhina ambao hawapo Zanzibar
kwa maslahi ya Wananchi bali wapo kwa maslahi yao binafsi. Na yote
haya yamekuja kutokana na Wazanzibar kupinga dhulma ya kuporwa kwa
Nchi yao.Wazanzibar wamechoka kutawaliwa na Tanganyika hivi kwa nini
hawaachiwi Wazanzibar wakaendesha mambo yao wenyewe.
Viongozi wa juu wa C.C.M wana kila sababu ya kuwadhulumu Wazanzibar
kwa vile wao hawana uchungu na Nchi na Raia wenyewe,wengi wao hawana
asili ya Zanzibar wamepandikizwa kwa maslahi ya Tanganyika. Viongozi
hao wanafaidika na jasho la Wazanzibar ndio maana Tanganyika kwa
kupitia maajenti wao wanafanya kila kinachowezekana kuikaba roho
Zanzibar hata kama damu ikimwagika basi wako tayari kwa hilo.
Tukimuangalia Rais wetu tokea hapo awali hakuwa na mvuto lakini pia
hao C.C.M wenyewe Zanzibar hawakumpa baraka zao. Kilichotokea ni
mabavu na kuwekwa kinguvu na Tanganyika hichi kitu kila mtu anaelewa.
Watanganyika walielewa kwamba kazi waliompa Dr Shein ataifanya
vilivyo. Wazanzibar kuna mengi bado yanakuja kupitia bwana huyu.
Kama ni hivyo sisi kama Wazanzibar tutegemee nini kwa mtu ambae nafasi
aliyonayo ni hidaya tu kutoka kwa Mtawala Tanganyika ! Shein kama
Shein yupo kwenye kiti kama Punda na hatamu aliebeba mzigo
anafuata ,hawashi wala hazimi.
Tumuangalie Seif Iddi naamini hata hilo jina ni la kupanga kwani yeye
binafsi hana hata hisia wala maji ya Uzanzibar. Amewekwa pale kuwa
kama ni usalama na balozi ambae anaiwakilisha Tanganyika na kutoa
Taarifa mihimu kwa kwa Tanganyika. Hapa ndio piukioni mwa fitina na
unyanyasaji kwa upande wa Wazanzibar.
Seif Iddi hayupo Zanzibar kama kiongozi lakini yupo kwa kufanya kazi
kama agenti na Muwakilishi wa Tanganyika. Wazanzibar wasishangae na
matusi wala fitina za Balozi huyu kwani yeye hana hasara hata
mukichinjana yeye tayari majumba yake ya fahari yako kwao
Bara,Zanzibar yuko kibaruani tu.
Mukitaka kujua udhaifu na unafiki wa Kiongozi huyu muangalieni kwenye
uchaguzi mdogo uliopita pale Bububu jinsi ya hisia zake,alishindwa
kujizuia na kutoa yale ambayo yamo kwenye moyo wake,chuki na fitina
kwa Wazanzibar.
Kiongozi ambae anashindwa kufuata maadili ya uongozi na badala yake
anawachochea Raia zake kufanya fujo na kupigana huku anapongeza na
kuwapa baraka zote Wahusika,kweli huyu ni kiongozi muaminifu ? Kweli
kama si agenti ni nani twambieni ?
Lakini pia hata Elimu yake haifanani na cheo chake.Inakuwaje yeye kama
Makamo wa Rais shughuli za Serikali ya Zanzibar azifanyie Tanganyika
kwenye Majumba yake binafsi pale Dar na nyingine kule Dodoma, jee
hakuna Zanzibar ofisi kwa Wageni kufikia na kupanga mipango ya Nchi ?
Hii ni kuonesha jeuri na ulwa alionao lakini akumbuke ya kwamba iko
siku ataulizwa na ajiandae na majibu hivi sasa.Sote tunaelewa kwamba
uongozi ni dhamana lakini pia hakuna refu lisilo na mwisho . Viongozi
wengi kama yeye wamepita na hivi leo hawatajwi tena ila kilichobaki
katika nafsi yao ni majuto na huzuni tu kwa yale walioyafanya.
Tujiulize kiongozi kama huyu ambae ana raslimali chungu mbovu kule
Tanganyika ambako ni kwao,kweli atawatetea Wazanzibar wanyonge
wanaodai haki zao hapa Zanzibar?Hivi kila siku tutapangiwa Maajenti
na Tanganyika na kutunyanyasa mpaka lini na kutuharibia udugu wetu wa
asili,hawa akina Seif Iddi ndio wanaoleta ubaguzi Zanzibar.
Angalieni michango ya maafa iliochangiwa ,ni Mzanzibar gani
aliefaidika ? Mtu kafiliwa na familia mzima anaenda kupewa ubani laki
moja wakati michango ya mabilioni imetolewa,hivi pesa hizi
zimetumikaje! Ndio maana Balozi huyu akawa na jeuri kwani mifuko yake
imetuna,kwa maana hiyo ana kila sababu kuwagombanisha Wazanzibar.
Tumuangalie Waziri Aboud ameingia katika medali ya siasa baada ya
kupata ngekewa ya vita vya panzi kupigana,yeye kama Kunguru Rais
Karume akampa nafasi. Mheshimiwa huyu hakufanya kosa akatia fitina na
baadae kujipendekeza Tanganyika.Kiongozi kama huyu lazima aabudu na
asujudu kwa mabwana zake,sishangai kuona anawachukia hata wale
watetezi wa uislamu na nchi yetu,analipa fadhila.
Mheshimiwa Aboud hana Elimu na ni dhahiri kwamba alifoji hata Elimu
yake na hili lipo wazi na ndio sababu hata ya kukosa nafasi ya
kupigania kiti cha Urais Zanzibar. Kama sio kashifa hii kuwa wazi wazi
basi leo hii Mohammed Aboud angekuwa ameshasimbikwa Urais kwani hapa
petu hatuchagui,tunasimbikiwa kutoka Tanganyika tu.
Lakini hili limefumbiwa macho na Tanganyika,kwa sababu Watanganyika
lengo lao sio mtu mwenye Elimu Zanzibar akawahangaisha bali wanahitaji
vihio wenye kupenda posho huku Tanganyika ikiendelea na biashara yake
"as usual".
Tuangalieni viongozi wengi katika Baraza la kutunga sheria wengi wao
hawana Elimu inayohitajika kwa nafasi walizopewa,inakuwaje mtu
kujifurahisha na kujitapa na Cheti cha ubaharia,hivi ubaharia na
utungaji wa sheria ni wapi na wapi ?Yote haya yamepangwa hayakuja
kibati mbaya,Tanganyika wanaelewa wanachokifanya.
Kweli kiongozi kama huyo atakuwa na uwezo wa kuitetea Zanzibar na
Wananchi wake au atukuwa yupo kwa maslahi yake binafsi huku akiitikia
hewala bwana,almradi posho inaingia. Hawa ndio wengi wa viongozi wetu
wanaoendesha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,hivi Wananchi wategemee
nini kutoka kwao isipokuwa matusi tu na kuiuza Nchi?
Kiongozi kama huyo kweli ataitetea Zanzibar awaudhi mabwana zake walio
mchagua na kumpa uwakala wa kuichuuza Zanzibar ? hilo haliwezekani
abadani ,na hawa ndio wengi wa viongozi wetu ndani ya Chama changu
nikipendacho cha C.C.M walivyo.Suala la mageuzi kwao ni mwiko hata
kama Zanzibar itaharikishwa na sababu kuwa ni wao basi wako tayari
kwa hilo.
Tumtupie macho Dk. Mwinyihaji na udokta wake na vikosi vyake anavyo
ongoza.Kwa kweli ni jambo la kushangaza kuona kwamba mawazo yake na
Elimu yake ni vitu tofauti.Anachojali ni maslahi binafsi yeye na
familia yake lakini uzalendo wa NCHI yeye hana kabisa. Zanzibar ni
Visiwa vidogo sana lakini ina vikosi vya ulinzi hata hayo Mataifa
makubwa Duniani hayana,hii inakuwaje lengo hapa ni dhulma tu.
Inapofika wakati ukaamrisha vikosi vyako vya ulinzi kuwashambulia Raia
wako wewe kama kiongozi unaipeleka Nchi yako wapi ? Kimawazo yangu ni
kwamba unazidisha uhasama ndani ya jamii ,lakini pia wewe kama
kiongozi na kiongozi wa Serikali utegemee kuona kama hichi
kinachotokea hivi sasa Zanzibar,vurugu na watu kuteswa bila sababu
kosa eti hawautaki Muungano sio haki!
Kinachoendelea hivi sasa Zanzibar ni mipango mahususi ilioandaliwa na
yeye akiwa ni muandaaji mkuu wa hayo. Elimu yake ni sawa na punda
aliebeba vitabu lakini maskini kilichoandikwa hakijui. Lakini pia cheo
na umri wake naona unamkanganya,anahisi ataishi milele,basi sheikh
wangu hukumbuki hata akhera yako ! mwisho wa yote ni wapi ? Hao
makachero uliwaleta kutoka Bara ni bure tu Wazanzibar wataendelea
kudai haki yao "for sure"
Sasa tuelekee kwa Waimarishaji wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar,hawa ni
akina Borafya,Shamte na wenzake hawana hata chembe ya
imani,ubinaadam,uungwana nathubutu kusema kwamba ni kondoo
waliopotea,hawana huruma kama wao ni miongoni mwa jamii watu. Maisha
yao yote ni hasadi,fitina na majungu huku wakifanya dhulma ya
kuwafitinisha Wazanzibar.
Umri wangu sio mdogo lakini tokea kuwa na akili yangu timamu sijawahi
kuona viongozi wa chama kufanya mikutano na kutukana matusi ya nguoni
bila kisisi chochote huku televisheni na vyombo vya habari vikionyesha
na kutoa habari hizo. Serikali ina washauri hivi kazi yao hao washauri
ni nini ? maanake ni dhahiri huku tunakoelekea kwa mtindo wa kina
Borafya ni kuelekea Jahhanam.
Hizi sio silka na tamaduni za Wazanzibar na mtu yeyote ambae utamuona
anafanya vitendo kama hivyo basi ujue huyo sio Mzanzibar bali ni mtu
wa kuja Visiwani na ana lake jambo,kufitinisha na kugombanisha kwa
maslahi maalumu au ametumwa kufanya hivyo kwa dhana na malengo
maalum,Wazanzibar tusikubali kuelekea huko,tupambane kiume.
Kamishina wa Polisi Zanzibar, Waswahili wana msemo unasema mcheza kwao
hutuzwa. Kamishina ni mtu ambae hajui hata uongozi ni kitu,hajui baya
wala jema,ni muongo na mnafiki hata sura yake tu ukimuona basi utajua
ni mtu wa aina gani.Anashindwa hata kupanga uongo wenye muelekeo.
Nilitegemea kuona kiongozi kama huyu anaheshimu cheo chake kama mlinda
usalama wa Raia lakini yeye amekuwa msimamiaji wa sera za akina
Borafya ndani ya C.C.M.
Kamishina huyu ni bendera inafuata upepo licha ya kufanya kazi
kisayansi lakini ni dhahiri kwamba kichwa chake kina uhaba wa Elimu.
Elimu yake na majukumu alopewa ni sawa na mbingu na ardhi kwa maana
hiyo sishangai sana na jinsi anavyowadhalilisha Wazanzibar wenzake.
Anachojaribu kukifanya ni kujikweza ili aweze kubakia kwenye nafasi
aliyopo kwani bila kuwa Mdhabi-dhabina na mnafiki kwenye Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Tanganyika basi wewe huna nafasi hili
linaeleweka.
Nimalizie kwa kusema kwamba Mchimba kisima huingia mwenyewe, Serikali
yetu imechimba Visima ihakikishe kwamba ikiwa haitakuwa makini basi
wataingia wenyewe kwani Wazanzibar wameshachoka na dhulma
zao.Uvumilivu una mwisho wake, hivi sasa Zanzibar imegeuka Paka
alofungiwa kwenye chumba na ameshajua kwamba anakufa kwa mateso,hana
budi na yeye kujihami kwa njia yeyote ile.
Kutokana na hili ilivyo ikiwa Dokta Shein ataendelea kuongozwa na Bara
kufuata ushauri wa Wahafidhina kama hivi anavyowafanyia Wazanzibar
basi na aelewe kwamba atayarishe mageraza mengi kama Firaun na
serikali zake lakini Wazanzibar hawatorudi nyuma tena kupigania haki
yaoya msingi,Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwanza.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments