Nipo Dodoma. Kilinachoendelea hapa ni mkusanyiko mkubwa wa wajumbe wa CCM kutoka pande zote za nchi yetu Tanzania. Mkutano mkuu wa 8 wa CCM unafanyika. Ni punde tu Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Jakaya Kikwete amabaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa amemaliza hotuba ya ufunguzi. Ni hotuba nzuri iliyojaa masuala ya msingi yahusuyo ujenzi wa chama endelevu na Taifa kwa ujumla wake. Hakika ni hotuba inayorejesha matumaini ya wana CCM ambayo kwa baadhi yao yalianza kupotea. Hakika CCM ni chama imara na madhubuti kweli kweli. Umoja na Mshikamano wa wananchana/ wajumbe wa chama wanaouonesha hapa ni ishara tosha kuwa chama hiki (CCM) kingali na UMOJA ambao ni dira ya Ushindi. Naam, kauli mbiu ya mkutano huu ni Umoja, Ushindi na Maendeleo. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI........ |
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments