[wanabidii] RIPOTI MAALUM: Mtandao wa Ufisadi, Siri Hadharani - Mwanzo

Tuesday, November 13, 2012

Miaka michache iliyopita iliibuka kashfa ndani ya chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo kwa kiasi kikubwa ilikitikisa na kukiyumbisha. Kashfa hiyo ilitokana na mkataba ambao ulitiwa sahihi na uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM na kampuni ya Bwana Subhash Patel kwa mintarafu ya kujenga jengo kubwa kuliko yote hapa Dar es Salaam (kwa sasa) kwa njia ya ubia kwenye kiwanja kilichopo kwenye kona ya barabara za Morogoro na Lumumba.

Ni dhahiri kuwa ufisadi hapa nchini Tanzania ni nadra kujulikana mpaka inapotokea wale wadau wa ufisadi husika wanapokorofishana. Hapo ndipo huwa 'mambo hadharani'. Vinginevyo, ukitegemea vyombo vya dola ndivyo vianike uoza basi utasubiri milele. Kwani inakisiwa kuwa mara nyingi navyo huhusika kwenye maovu hayo au katika kuyaficha.

Sasa kashfa hii iliibukaje hadharani? Kashkash hii ilianza pale mwanachama wa CCM mwandamizi Bwana Nape Nnauye alipotaka kugombea uenyekiti wa UVCCM yaani Umoja wa Vijana wa CCM Taifa. Majungu yakaanza na jina lake kufutwa na hapo ndipo kisu kikafika mfupani. Nape akatangaza hadharani kuwa kuna ufisadi mkubwa ndani ya UVCCM na ndio maana jina lake limefutwa.

Nape akatema cheche, 'Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya UVCCM Bwana Edward Lowassa, (Waziri Mkuu aliyejiuzulu kutokana na kashfa ingine ya ufisadi ya Richmond) pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM (wa wakati ule) Bwana Emmanuel Nchimbi ndio waliosaini mkataba kwa upande wa UVCCM kuingia ubia na Subhash Patel'. Alisema mkataba huo ulisainiwa kinyemela na haukupitishwa na mamlaka halali za UVCCM. Aidha, mkataba huo ulimpendelea mno mno Subhash na hata kufikia mahali Subhash akabidhiwe jengo la UVCCM ili aliweke dhamana ili akope benki kwa ajili ya ujenzi huo. Yaani ni kisa cha kumkaanga samaki kwa mafuta yake!


http://wotepamoja.com/archives/10342#.UKIQZdU990A.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments