Naomba kuchukua fursa hii kuwajulisha kuwa uongozi wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDASA) wameandaa kongamano la kitaifa siku ya tarehe 9 Desemba, litakalofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV.

Lengo kuu la UDASA ni kuamsha mjadala wa kitaifa kujaribu kuangalia mwelekeo wa kitaifa kwa miaka mingine hamsini ijayo. Yapo mambo ambayo sisi kama taifa tunahitaji kuyajadili kwa uwazi na upana zaidi kwa lengo la kujenga mustakabali wetu kwa siku za mbeleni. Hivyo, kwa niaba ya uongozi mzima wa UDASA, napenda kuwajulisheni kuwa nia yetu ni kutaka kongamano hilo liwe la kitaifa kwa kuwa na mchanganyiko wa kila tabaka na kundi la watanzania kwaajili ya kuanzisha mjadala utakaosambaa zaidi wenye lengo la kufanya tathmini wapi tumekosea na namna gani tufanye kama taifa ili tuliepushe taifa letu na majanga makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
a) Mwelekeo wa hali ya siasa na demokrasia yetu
b) Hali ya elimu na maendeleo ya taifa letu
c) Hali ya amani na utulivu wa taifa letu kwa miaka ijayo
d) Mchango wa rasilimali za taifa kwa maendeleo ya taifa
e) Maswala mengineyo yenye maslahi kwa taifa kama vile afya, ulinzi, miundombinu nk.
d) Mchango wa rasilimali za taifa kwa maendeleo ya taifa
e) Maswala mengineyo yenye maslahi kwa taifa kama vile afya, ulinzi, miundombinu nk.
Hivyo, kwa wale watakaopenda kuwa nafasi maalumu ya kuzungumza miongoni mwa mada hizo hapo juu awasiliane nami kwa email: farajalugome@yahoo.co.uk au farajalugome@gmail.com. Jambo la msingi aniambie kwa kifupi angependa aongelee kuhusu nini, nasi tutamjulisha. Tunahitaji kuwa na michango mingi ili tuweze kuwa na mawazo mapana zaidi na kuufanya mjadala uwe huru zaidi na wenye manufaa kwa taifa.
Asante sana.
Mr. Faraja Kristomus (Katibu - UDASA)
Department of Foreign Languages and Linguistics
University of Dar es Salaam
P.O.Box 35040, Dar es Salaam
Tanzania
Mobile: +255 787 52 53 96 / +255 717 086 135
Department of Foreign Languages and Linguistics
University of Dar es Salaam
P.O.Box 35040, Dar es Salaam
Tanzania
Mobile: +255 787 52 53 96 / +255 717 086 135
"All human beings are equal except our beliefs, tribes and thinking, which are always accidents and never the essences of our humanity. We acquire them after getting out of the wombs of our mothers".
0 Comments